Friday, January 11, 2013

WAHARIRI NA BARAZA LA HABARI WATEMBELEA VITENGO VYA TUME YA KATIBA


 Katibu wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Bw. Assaa Rashid (wa pili kulia), akitoa ufafanuzi uhifadhi wa maoni ya maandishi yanawasilishwa na wananchi katika Tume kwa wadau wa Taasisi za Habari nchini waliotembelea ofisi za Tume leo (Januari 10, 2013). Taasisi zilizotembelea Tume ni Baraza la Habari Tanzania (MCT), Chama cha Wamiliki wa Vyombo vya Habari (MOAT), Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake (TAMWA) na Jukwaa la Wahariri (TEF).
 Mjumbe wa Sekretarieti ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Bw. Mohammed Khamis Hamad akitoa ufafanuzi kuhusu mfumo wa uchambuzi wa maoni ya wananchi kwa Ujumbe wa Taasisi za Habari nchini uliotembelea ofisi za Tume leo (Januari 14, 2013). Taasisi zilizotembelea Tume ni Baraza la Habari Tanzania (MCT), Chama cha Wamiliki wa Vyombo vya Habari (MOAT), Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake (TAMWA) na Jukwaa la Wahariri (TEF).
Mjumbe wa Sekretarieti ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Bi. Hanifa Masaninga akitoa ufafanuzi kuhusu uandaaji wa maoni ya wananchi na kuwa Kitengo cha Taarifa Rasmi (Hansard) kwa ujumbe wa Taasisi za Habari nchini waliotembelea ofisi za Tume leo (januari 10, 2013). Taasisi zilizotembelea Tume ni Baraza la Habari Tanzania (MCT), Chama cha Wamiliki wa Vyombo vya Habari (MOAT), Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake (TAMWA) na Jukwaa la Wahariri (TEF).
Picha na Tume ya Katiba.

No comments:

Post a Comment