Saturday, January 12, 2013

DIWANI WA CCM AKAMATWA KWA TUHUMA ZA MAUAJI YA KUKATA WANAWAKE VICHWA

DIWANI WA CCM AKAMATWA KWA TUHUMA ZA MAUAJI YA KUKATA WANAWAKE VICHWA


Na Anthony Mayunga-Musoma
Januari 10,2013.

JESHI la polisi mkoani Mara linamshikilia diwani wa kata ya Mgango

wilayani Butiama Wandwi Maguru(34)(CCM) akihusishwa na tuhuma za
mauaji ya mama mmoja aliyekatwa kichwa wilayani humo.

Kamanda wa polisi mkoa wa Mara Absalom Mwakyoma amethibitisha
kukamatwa kwa diwani huyo na kufanya jumla ya watu ambao
wameishakamatwa kuhusiana na mauaji hayo kufikia 15.

Amesema anahusishwa na mauaji ya mwanamke mmoja Taabu Makanja
aliyeuawa desemba 21,2012 kwa kukatwa kichwa na wahusika wakakindosha
baada ya kufukuzwa na wananchi.

Mwakyoma amebainisha kuwa mama huyo mkazi wa kijiji cha Kwibara
wilayani Butiama alivamiwa na kundi la watu,kisha akauawa kwa kukatwa
kichwa ambapo wananchi walipiga yowe na wahusika wakawa
wamekitelekeza.

“Kukamatwa kwake kunatokana na ushirikiano wa vyombo vya uchunguzi
kutoka makao makuu ya jeshi la polisi,na wengineo ambapo wananachi
wanajitokeza kutoa ushirikiano”alisema.

Amesema jumla ya watu 15 wameishakamatwa kuhusiana na mauaji
yanayoendelea mkoani humo ambapo watu 4 wameishafikishwa mahakamani.

Alisema uchunguzi ukikamilika atafikishwa mahakamani,na kuomba
wananchi waamini jeshi hilo kwa kulipa ushirikiano ili kukomesha
vitendo vya kikatili vinavyofanywa na kundi la watu wachache.

No comments:

Post a Comment