Sunday, January 6, 2013

PHILIPO MULUGO AZINDUA OFISI YA WAENDESHA BAJAJI NA KUCHANGIA ZAIDI YA SHILINGI MILIONI MOJA KUTUNISHA MFUKO WAO WA KUSAIDIANA

Naibu waziri wa elimu na mafunzo ya ufundi Philipo Mulugo akikata utepe kuzindua na kufungua ofisi ya waendesha bajaji mkoa wa Mbeya eneo la isanga
Naibu waziri Mlugo akishangiliwa na wanachama wa chama cha waendesha bajaji mkoa wa Mbeya mara baada ya kuzindua ofisi yao
Katibu mkuu wa chama cha waendesha bajaji mkoa wa mbeya Ernest Mwaisango akisoma risala kwa mgeni rasmi
Mwenyekiti wa chama cha waendesha bajaji Iddi Ramadhani akimkaribisha mgeni rasmi
Kabla ya kuanza kuhutubia Mweshimiwa Mulugo akimkabidhi hundi ya shilingi milioni moja mwenyekiti wa waendesha bajaji Iddi Ramadhani ilikuboresha mfuko wao wakusaidiana
Mulugo akimkabidhi mwenyekiti wa waendesha bajaji jumla ya shilingi laki nne kwa ajili ya kulipia kodi ya ofisi kwa mwaka mzima
Pia mweshimiwa Mulugo alitoa kiasi cha shilingi laki tano kwa chama cha waendesha bodaboda mkoa wa mbeya hapa akipena mkono na makamu mwenyekiti wa chama hicho Fredy Mwambene
Nae mc na mwandishi wa habari Chales Mwakipesile mwenye suti ameahidi kukipatia chama hicho kompyuta ya kisasa
Hapa mweshimiwa Mulugo akishirikiana na waendesha bajaji katika kucheza na kufurahia uzinduzi wa ofisi hiyo

Mweshimiwa naibu waziri wa elimu na mafunzo ya ufundi akiwahutubia wananchi waliofika katika uzinduzi huo
Safari ya kwenda kupumzika imewadia anarudishwa na bajaji hadi kwakwePicha Kwa Hisani ya Mbeya yetu Blog

No comments:

Post a Comment