Friday, September 21, 2012

BENKI YA KCB YATOA MSAADA KWA HOSPITALI ZA AMANA NA MWANANYAMALA

PICHA NA HABARI JUMA KAPIPI


Mkuu wa Kitengo Mauzo na Huduma kwa wateja na Jamii  wa benki ya KCB  Tanzania ,Christina Manyeye, akiwa amemshika mmoja wa watoto wenye umri wa siku moja waliozaliwa katika wodi ya wazazi ya Amana jijini Dar es Salaam, wakati alipotembelea waodi hiyo, baada ya kutoa msaada wa Mashuka 116 na Mashine ya joto ya kutunzia watoto wanaozaliwa kabla ya wakati wake  ( Baby Warmer Mashine) Vitanda Vitano vya kujifungulia akina mama wajawazito vvyote vikiwa na thamani ya shilingi Milioni 15.640.000.Vilivyotolewa na Benki ya KCB Tanzania.

Mkuu wa Idaraya ya Uhazini wa beki ya KCB Tanzania Sam Kimath akimkabidhi msaada wa Mashuka 116  Mganga Mkuu wa Manispaa ya Ilala Asha Mahita, na Diwani wa kata ya Ilala Edson Fungo wakati wa hafla iliyofanyika jijini Dar es salaam, jumla ya vifaa mbalimbali vyenye thamani ya shilingi Milioni 15,640,000. Vilitolewa msaada na benki hiyo kwa ajiri ya kusaidia hospitali hiyo ya Amana. Kushoto ni Mkuu wa Kitengo Mauzo na Huduma kwa wateja na Jamii  wa benki ya KCB Christina Manyeye.

Mkuu wa Idaraya ya Uhazini wa beki ya KCB Tanzania Sam Kimath akimkabidhi msaada wa Mashuka 116  Mganga Mkuu wa Manispaa ya Ilala Asha Mahita, na Diwani wa kata ya Ilala Edson Fungo wakati wa hafla iliyofanyika jijini Dar es salaam, jumla ya vifaa mbalimbali vyenye thamani ya shilingi Milioni 15,640,000. Vilitolewa msaada na benki hiyo kwa ajiri ya kusaidia hospitali hiyo ya Amana. Kushoto ni Mkuu wa Kitengo Mauzo na Huduma kwa wateja na Jamii  wa benki ya KCB Christina Manyeye.

 Mkuu wa Kitengo Mauzo na Huduma kwa wateja na Jamii  wa benki ya KCB Christina Manyeye, akimkakabidhi  Mganga msaidizi wa Hospitali ya Mwananyamala DR.chrispian Kayola  Mashine ya Kutunzia joto ya watoto wanaozaliwa kabla ya muda,(babyWarrmer Machine) yenye thamani ya shilingi Milioni 7.8.iliyotolewa na Benki ya KCB Kwa ajili ya kusaidia jamii inayopata huduma katika hospitali hiyo.wanao shuhudia ni Diwani wa kata ya Ilala Edson Fungo na Mganga msaidizi wa Hospitali ya Amana DR.Shaany Mwaruka. Hafla hiyo ilifanyika katika Hospitali ya Amana jijini Dar es Salaam.



Na Mwandishi Wetu

 
Benki ya KCB Tanzania, imetoa msaada wa vifaa  kwa wodi ya akina mama wajawazito


vyenye thamani ya shilingi milioni 15,640,000 kwa hospitali  ya  Amana katika uzinduzi wake wa   wiki ya jamii.
 

Akizungumza katika hafla fupi ya mabidhiano ya vifaa hivyo  yaliyofanyika hospitalini hapo,  Mkuu wa kitengo cha masoko na jamii wa benki ya KCB Christine Manyenye  alisema  Msaada huo unalenga kupunguza vifo vya akina mama na watoto. 

Manyenye  alisema, Benki ya KCB inatambua umuhimu wa  afya ya mama na mtoto na ndiyo maana iliona kuwa ni jambo zuri kuelekeza msaada huo muhimu kwa kundi hilo Kila mwaka. 

"Kwa kawaida tunaangalia sehemu yenye mahitaji sana msaada na kutoa mchango  sehemu hiyo, Kwa mfano tumegundua kuwa hospitali zetu haswa hizi zinazohudumia watu wenye kipato cha chini zina matatizo mengi na ndiyo maana leo tumekuja kutoa mchango hapa Amana,alisema Manyenye

"Ni matumaini yetu kuwa, vifaa hivi vilivyotolewa na Benki ya KCB vitachangia kwa kiasi kikubwa kuboresha utoaji huduma kwa akina mama na watoto na hivyo kujenga taifa lenye jamii ya watu wenye afya bora," aliongeza.
 

Mwakilishi wa mganga mkuu wa hospitali hiyo  Dokta Shani Mwaruka aliishukuru Benki ya KCB kwa msaada huo na kusema kuwa utasaidia  kuboresha huduma kutokana na kupatiwa vifaa hivyo.

"Hali za hospitali zetu hizi za serikali siyo nzuri sana kutokana na ukosefu wa vitendea kazi, hakika tunahitaji msaada ili tuweze kutoa huduma bora na ndiyo maana tunatoa shukrani za pekee kwa benki ya KCB, alisema Dk.Shani

Vifaa vilivyotolewa ni pamoja na mashine ya joto kwa watoto wachanga waliozaliwa bila kutimia, vitanga vya kujifungulia 5, vifaa vya kusaidia wakati wa akina mama wajawazito kujifungua 10, mashuka 116, drums 20 na Cord clamp 100.

MWANANYAMALA

Hospitali ya Mwananyamala jijini Dar es Salaam, jana ilipokea msaada wa mashine ya joto kwa watoto waliozaliwa bila kutimia (baby warmer )  yenye thamani ya shilingi 7,850,000 kutoka katika Benki ya KCB Tanzania.


 Akizungumza wakati wa makabidhiano ya msaada huo, mkuu wa kitengo cha masoko wa benki hiyo Christine Manyenye  alisema msaada huo umetolewa baada ya kubaini uwezo mdogo wa hospitali za umma kuhudumia watoto wanaozaliwa bila kutimia (pre mature) 

"Kabla ya kufukia uamuzi wa kutoa msaada huu tulichunguza na kugundua kuwa huduma kwa watoto waliozaliwa kabla ya muda wao wa kuzaliwa bado si nzuri kutokana na ukosefu wa vifaa hivyo tuliona ni jambo zuri kuelekeza msaada wetu kwa kundi hili" alisema Manyeye huku akibainisha  kuwa benki ya KCB imekuwa ikielekeza zaidi misaada yake kwenye makundi yenye mahitaji  makubwa na yenye uchache wa rasilimali za kutatua matatizo za aina mbalimbali.

Kwa upande wake Mwakilishi wa mganga mkuu wa hospitali hiyo  ya Mwananyamala Dokta Chrispian Kayolai aliishukuru Benki ya KCB kwa msaada huo na kusema kuwa utasaidia kwa kiasi kikubwa kuboresha huduma kwa watoto wanaozaliwa kabla ya muda wao.


"Tunachangamoto nyingi ambazo tunakutana nazo wakati wa kutoa huduma na haswa kwa ajili ya vitendea kazi,Msaada huu tumeupokea leo utasaidia sana kuboresha huduma na tuna kila sababu ya kuishukuru sana benki ya KCB," alisema Dk Kayolai

Kwa mujibu wa Manyenye, katika kuadhimisha wiki ya jamii hospitali za KCMC Moshi, Mwembeladu Zanzibar, Morogoro na Mount Meru ya Arusha itanufaika na misaada itakayogharimu shilingi milioni 79,040,000/-

No comments:

Post a Comment