Wednesday, September 12, 2012

MAANDAMANO DAR,WAANDISHI WAMPIGA STOP WAZIRI NCHIMBI KUHUTUBIA

Mhariri mtendaji wa Channelten Dinna Chahali akizungumza katika maandamano hayo kuhusu mauaji ya mwandishi wa Channelten mkoani Iringa Daudi Mwangosi.

 MEENA
Waandishi wa habari jijini Dar wakiandamana kulaani mauaji ya Daudi Mwangosi aliyeuawa kikatili kwa kupigwa bomu tumboni

Hapa waandishi wakijaribu kuonesha ni jinsi gani wanavyopata taabu wakati wa kufanyakazi zao ambazo sasa zimesababisha mauaji yasiyo ya lazima kwa Daudi Mwangosi


Raisi wa Muungano wa Klabu za waandishi wa habari nchini UTPC Bw.Keneth Simbaya akizungumzia kulaani mauaji ya Daudi Mwangosi anayedaiwa kuuawa kwa kupigwa bomu na askari Polisi akiwa katika kazi zake huko mkoani Iringa.

Hivi ndivyo waandishi walivyoanza maandamano yao katika ofisi za Channelten jijini Dar kufuatia kulaani mauaji ya Daudi Mwangosi aliyeuawa kwa kupigwa bomu tumboni wakati akiwa kazini.

No comments:

Post a Comment