Wednesday, September 12, 2012

KILA KATA KUSHIRIKI CHALLENG CUP TABORA



Na Lucas Raphael,Tabora
SOKA 
MDAU  wa mchezo wa soka,mkoani Tabora,ambaye ameanzisha mashindano ya kombe la Godfrey Kasanga Challenge Cup, Godfrey Kasanga,amesema baada ya kufanikiwa katika kombe hilo kwa kushikisha kila kata, sasa amegeukiwa mashindano kwa mchezo wa mpira wa pete.
Kasanga alisema hayo wakati akifanya mazungumzo na gazeti hili,mwanzoni mwa wiki hii.
Alisema licha kuweka progaramu zake vizuri,na kufanikiwa sana kwenye mashindano ya kombe la Godfrey Kasanga Challenge Cup,sasa kombe hilo pia naanzisha kwa upande wa netiboli, ili kuinua vipaji kwa upande huo wa jinsia.
Kasanga alisema mtindo alioutumia kwenye mashindano ya upande wa wanaume ndiyo atakaoutumia kwa wanawake na kwamba zawadi hazitapishana sana.
Aliongeza kuwa siku za kuanza kwa mashindano ya mpira wa pete,atayatangaza hivi karibuni baada ya kufanikisha miapngo ya udhamini.
Katika hatua nyingine mdau huyo alisema,pamoja na kuanzisha mashindano hayo,pia natarajiwa kutoa motisha kwa makocha wa mpira wa soka na pete ili kuweza kutoa nafasi ya watalaamu hao kuibua vipaji zaidi na kuipenda kazi yao.
“Kutangaza mashindano pekee haitoshi…..kinachotakiwa sasa ni kuangaliwa kwa makocha katika suala la motisha kwani hili nina imani kubwa litasaidia kupata timu zitakazokuwa zinapatiwa mafunzo na makocha wetu.”alisema Kasanga.

Alisema alifanikiwa sana kwenye mashindano ya kombe aliloanzisha kwa upande wa wanaume,na kwamba safari hii anatarajia kutafuta udhamini mkubwa zaidi kwa kuboresha zawadi kwani kwa mashindano yaliyopita alitumia fedha zake za mfukoni.
Hata hivyo alisema mashindano ya upande wa wanawake kwa maana ya mpira wa pete,alisema atajikita zaidi maeneo ya kata za mjini kwani hana imani kama vijijini atafanikiwa kupata timu kadhaa zitakazoshiriki kombe hilo.
Aidha alisema na kusisitiza kuwa atawasihi viongozi wa pande zote mbili katika michezi ya soka na pete ili kuweza kuona ni jinsi gani mashindano hayo yanaweza yatakuwa na mvuto na kuweza kupata wadhamini watakaonogesha zaidi.
“Lakini bado napenda kutoa wito zaidi kwa wadau wa soka mkoa Tabora,wajitokeze zaidi kuniunga mkono ili mipango nitakayoianzisha ifanikiwe na kuweza kurejesha Tabora iliykuwa  na timu ambazo hadi leo zimeweka rekodi ya kimichezo.
Alisema hadi sasa amejipanga vya kutosha na muda siyo mrefu mashindano aliyoanzissha yataanza kurindima na kuwataka wakzazi wa Tabora wakae mkao wa kula na burudani tosha.

Mwisho-




No comments:

Post a Comment