Tuesday, September 11, 2012

WAKAMATWA NA MAZAO YA MISITU YAWAFIKIHSHA MAHAKAMANI

 Na, Lucas Raphael,Tabora.

TISA WAFIKISHWA MAHAKAMANI KWA KUKUTWA NA MAZAO YA MISITU.

Watu tisa waliokamatwa wiki iliyopita wakiwa na mazao ya misitu ndani
ya pori la akiba la Kigosi  wakiwemo askali wawili wa jeshi la
wananchi wa Tanzania - JWTZ wamefikisha mahakama ya hakimu mkazi wa
mkoa wa Tabora wakikabiliwa na mashitaka mawili kila mmoja.

Katika kesi ya kwanza inayowakabili watu watatu cpl Moshi Jumanne, cpl
Mustafa Yusuph na Sophia Shigemela ilidaiwa mbele ya hakimu mkazi wa
mahakama ya mkoa Hamis Bally kuwa walitenda makosa hayo mawili tarehe
07-09-2012 katika kijiji cha Mnange wilaya ya Kaliua.

Upande wa mashitaka ukiongozwa na wakili wa serikali Rwegire
Deusdedit ulisema kuwa siku hiyo majira ya saa za usiku washitakiwa
walikutwa wakimiliki  kinyume cha sheria mbao 633 mali ya serikali
bila kuwa na kibali au reseni.

Wakili Rwegire alidai katika shitaka la pili kwamba siku hiyo
washitakiwa walikamatwa wakisafirisha mazao hayo ya misitu yenye
thamani ya tshs 6,330,000/= kwa kutumia gari lenye namba za usajiri
5659 JW 09 mali ya jamuhuri ya muungano bila kuwa na kibali.

Washitakiwa wote watatu walikana makosa hayo na wapo nje kwa dhamana ya mtu mmoja kwa ahadi ya  tshs milioni moja kila mmoja ambapo kesi
hiyo imeahirishwa hadi tarehe 08/10/2012 kwani upelelezi badohaujakamilika.

Katika kesi ya pili inayowakabili watu sita Rchard Samwel,Gasper
Kagutwa, Sultan Hadan, Mashiba Lugaka, Msina John na Kiwele William
ilidaiwa kuwa washitakiwa walitenda makosa yao tarehe 07-09-2012
katika kijiji cha mwendakulima wilaya ya Kaliua Mkoani Tabora.

Wakili wa serikali Rwegire alidai mbele ya hakimu mkzai Bally kuwa
siku hiyo watuhumiwa wote sita walikutwawakimliki mbao 422 kinyume cha
sheria kwani hawakuwa na kibali.

Akiwasomea shitaka la pili wakili wa serikali alidai mahakamani hapo
kuwa siku hiyo washitakiwa walikutwa wakisafirisha mazao hayo ya
misitu yenye thamani ya tshs 4220,000/= kwa ktumia gari lenye namba za
usajiri T761 BCV aina ya fusso.

Washitakiwa wote walikana mashitaka yao na mahakama iliwataka walete
wadhamini wawli wawili kwa kila mmoja ili weweze kuwadhamini kwa ahadi
ya shilingi milioni mbili na keswi hiyo ilihairishwa haditarehe 24
mwezi huu itakapotajwa tena.

MWISHO.


No comments:

Post a Comment