Wednesday, September 12, 2012

SUMATRA MARUFUKU KUPANDISHA NAULI HOLELA


Na Lucas Raphael,Tabora
Sumatra kuchukua hatua kali kwa wanaopandisha nauli holela
Mamlaka ya udhibiti wa usafiri wa majini na nchi kavu Sumatra Mkoani Tabora imewatahadhalisha wamiliki wa vyombo vya usafiri kutopandisha nauli kiholela bila kuwasiliana na taasisi hiyo vinginevyo watachukuliwa hatua kali za kisheria.
Akizungumuza na gazeti hili Meneja Mawasiliano kwa umma mkoani hapa David Mziray alisema kuwa baadhi ya wamiliki wa vyombo vya usafiri hususani mabasi yanadaiwa kupandisha nauli kiholela hali ambayo wananchi ambao ni watumiaji wa vyombo hivyo wanapati adha kubwa.
Alisema kuwa sheria kali zitachukuliwa kwa waleote ambao watapandisha nauli hizo kiholela bila kufuata taratibu za upandishaji nauri ikiwa na kupigwa faini.
Alisema wamiliki hao endapo wanataka kupandisha nauri hizo wafuate utaratibu ambao utawawezesha kupandisha nauri hizo kwa kuzingatia umbali wa sehemu pamoja na misingi ya dhamira hiyo.
Baadhi ya wananchi wilayani Nzega wakizungumuza kwa nyakati tofauti wameilalamikia Sumatra kwa kuchelewa kuchukua hatua mapema za upandishaji nauri ki holela kwa wamiliki wa vyombo hivyo.
Wasema kuwa nauri inayo tozwa kutoka tabora mpaka nzega shilingi 15000,Igunga nzega shilingi 4000 pamoja na sehemu mbalimbali mkoani hapa.
Wakifafanua kuwa awari ya hapo nauri ilikuwa shilingi 6000 Tabora –Nzega huku Igunga- Nzega shilingi 3000 wameiomba serikali kuingilia kati  suala hilo.
Baadhi ya wapiga debe wa vyombo hivyo katika stendi kuu ya basi walisema kuwa chanzo kikuu cha kupandisha nauri hiyo ni kutokana na kuwepo kwa kila abilia awe amkee(leave seat).
‘’Walisema kuwepo kwa leave seat ndiko kumepandisha nauli hiyo kweli hatuwatendei haki abiria hawa hivyo na hali hii ipunguzwe ili hali iwe sawa kwani hali ni gumu’’alisema mpiga debe mmoja.

Mwisho.

No comments:

Post a Comment