Monday, September 10, 2012

RED CROSS NZEGA KUCHANGISHA DAMU KWA WANANCHI

Na Lucas Raphael,Nzega

CHAMA cha Msaraba Mwekundu wilayani nzega Mkoani Tabora kinatarajia kuanza kuchangisha damu kwa wanachama wake ili kuondoa tatizo la upungufu wa dama katika Hospitali ya wilaya Nzega.

Kauli hiyo imetolewa baada ya Hospital ya wilaya ya Nzega kuwa na tuhuma za kuuza damu kwa wananchi mpaka kupelekea baadhi ya wagonjwa kupoteza maisha yao.

Akizungumuza katika uzinduzi wa chama hicho jana Mwenyekiti wa chama hicho wilaya ,Gabriel Gibson alisema kuwa chama hicho kimejipanga kutoa Elimu ya utoaji damu kwa wana chama wake pamoja na wananchi.

Lengo la kutoa damu ni kutaka kukabiliana na upungufu wa damu uliopo katika Hospitali ya wilaya ya Nzega na kuwa saidia wananchi watakao bainika wana upungufu wa damu.

Aliwataka wananchi kwa ujumla wilayani hapa kukipokea kwa mikono miwili chama hicho cha msaraba mwekundu ilikiweze kuleta uzalendo kwa wananchi na kurejesha nyuma upendo kwa jamii husika tofauti.

Akitoa angalizo kwa wananchama watakao jiunga katika chama hicho kuwa wasiingie kwa masirahi yao binafsi bali waingie kwa kujitolea kwa jamii ilikuweza kuleta ufanisi zaidi katika kujitolea kwa shuguli mbalimbali za kijamii.

Mkuu wa wilaya ya Nzega Bituni Msangi ambaye ni mlezi wa chama hicho alisema kuwa wananchi wanapaswa kujitolea katika kuchangia damu pindi zoezi hilo litakapo anza kupitia chama hicho.

Aliongeza kuwa chama hicho nichaki jamii zaidi hivyo wanapaswa kujitolea zaidi na kuwa wazaledndo kwa nyakati tofauti ili kuleta upendo katika jamii pamoja na kutoa misaada mbalimbali ya kijamii ikiwepo na majanga ambayo hutokea mara kwa mara katika jamii husika.

Mratibu wa chama hicho wilaya ,Liliani Kuhasi akitoa angalizo alisema kuwa dam itakayo changwa na wananchi itatunzwa kwa uangalifu pamoja na matumizi sahihi ya wagonjwa watakao hitaji hudum hiyo muhimu na kuongeza kuwa ulinzi mkali utaimalishwa katika utunzaji wa dam hiyo.

Mwisho.

No comments:

Post a Comment