Wednesday, September 19, 2012

WATAALAM WA MAABARA WATAKIWA KUTOCHANGANYA SIASA NA TAALUMA YAO


WATAALAM WA MAABARA WATAKIWA KUTOCHANGANYA SIASA NA TAALUMA YAO
 Na Lucas Raphael,Tabora
WATAALAM wa Maabara za tiba Tanzania (MeLSAT), wametakiwa kutojiingiza katika mambo ya Siasa na badala yake wajikite zaidi katika kazi yao ya kutoa huduma kwa wagonjwa.
Wito huo ulitolewa na mkuu wa mkoa wa Tabora Bi Fatuma Mwassa wakati akifungua kongamano la 26 la Sayansi na mkutano mkuu wa mwaka wa chama cha wataalam wa Maabara za tiba Tanzania uliofanyika katika ukiumbi wa chuo cha utumishi wa umma mjini Tabora.
Bi Mwassa alisema kwamba kwa mtaalam wa maabara kujihusisha na Siasa ni kutoitendea haki jamii, hivyo akawataka kuacha maramoja kujihusisha mambo ya siasa ili kuongeza ufanisi kazini kwa kuwahudumia wagonjwa kikamilifu.
“Mimi huwa inauma sana wanasayansi kujiingiza katika msuala ya siasa, na nilikuwa nasubili mahala pa kusemea, sasa leo nimepata sehemu hii napenda sana nisisitize jambo hili, achani kabisa kutamani siasa, mtaua watu ninyi ni watu muhimu sana kwa taifa” alisisitiza Bi Mwassa.
“Ndugu wanasayansi nawaomba sana mpiganie taaluma yenu msije mkajiingiza kabisa kwenye mambo ya haya ya kisisa” alisema mkuu huyo wa mkoa.
Aidha mkuu huyo wa mkoa alisema kuwa kongamano hilo liwe chachu ya kuleta mabadiliko katika sekta ya mabara za tiba hapa nchini na kwamba wataweza kupata fursa ya kubadilishana uzuefu, kuwajengea uwezo zaidi wa kuwahudumia wagonjwa pamoja na kujadili changamoto zinazowakabili sehemu zao za kazi.
“Taaluma ya mtu wa maabara ni mhimu sana kwa wagonjwa maana hawezi kwenda kwa daktari kutibiwa bila kupitia kwa mtaalam wa kupima magonjwa” alisema Bi Mwassa.
Mkuu huyo wa mkoa alisema kwamba, kwa kuwa wataalam wa maabara ni msingi wa kupata tiba kwa mgonjwa, hivyo hawana budi kufanya kazi kwa bidii ili jamii iweze kupata huduma hiyo muhimu kikamilifu.
Aliwataka kuimarisha uhusiano na kuongeza ubunifu sanjali na kutafuta fursa pamoja na kuzitumia vivuri katika maeneo yao ya kazi, kwa lengo la kuboresha huduma za uchunguzi katika hospitali wanazofanyia kazi.
Awali Rais wa chama cha wataalam wa maabara za tiba hapa nchini Bw. Sabas Mrina alisema kwamba kongamano hilo limelenga zaidi kuimarisha ushirikiano ili kuendelea kutoa huduma bora zaidi kwa jamii wanayoihudumia.
Alisema kuwa pia kongamano hilo limelenga kuleta ushirikino baina ya madaktari na wataalam wa maabara za  tiba, lengo likiwa ni kuongeza ufanisi kwa kutoa huduma hiyo muhimu kwa wagonjwa.
Mwisho


No comments:

Post a Comment