Friday, September 14, 2012

CCM WAWASILISHA RUFAA MAHAKAMA KUU TABORA

NA Lucas Raphael,Igunga.



C
HAMA chama mapinduzi ccm wilayani Igunga Mkoani Tabora jana kimethibitisha kupeleka kusudio la kutaka kukata rufaa katika mahakama ya Rufaa dhidi ya kupinga maamudhi ya mahakama kuu kanda ya tabora yaliyotengua ubunge wa Dkt,Peter kafumu aliyekuwa mbunge wa jimbo la Igunga.





Akizungumuza na gazeti hili Katibu wa chama cha mapinduzi ccm wilaya mery maziku alisema kuwa tayari kusudio hilo limepelekwa kwa chama cha demokrasia na maendeleo chadema pamoja na mahakama kuu ya rufaa.

Katibu huyo alisema kuwa kazi hiyo imefanywa na mawakili wa Dkt,Kafumu kufanya taratibu hizo.

Akizungumza kwa harahara katibu huyo alisema kuwa taarifa zaidi zitatolewa juu ya rufaa hiyo kwani kwa kipindi hicho alikuwa akiwahi katika mkutano wa hadhara wa chama hicho.

’’taarfa zaidi tutawapatia lakini kwa kifupi unayouliza hayo ni kweli yote tumefanya hivyo na taarifa hizoi viongozi wa chadema wanazo’’.alisema katibu huyo.

Taarifa za uhakika kutoka ofisi ya wakili wa kafumu zinasema kuwa tayari taratibu zote za kupeleka kusudio hilo la kukata rufaa kwa mteja wao zimefanyika kwa mawakili wa mlalamikaji Joseph kashindye.

Taarifa hizo zinaeleza kuwa mwanasheria mkuu wa serikali pamoja na msimamizi wa uchaguzi taarifa wanazo na kuongeza kuwa hoja za msingi zitapelekwa katika mahakama ya rufaa ndani ya siku 30 ili kuepuka upotevu wa muda.

Wakili Safari

Profesa Abdalla Safari aliyekuwa wakili wa mlalamikaji Joseph kashindye alikili kupokea taarifa hizo za kusudio la kutaka kukata rufaa.

Alisema kuwa ni haki ya kila mtu kukata rufaa endapo hajalidhika na maamuzi ya awari lakini Abdalla alikitaka chama cha mapinduzi kisiwapotezee muda wananchi wa Igunga kwani kesi hiyo ni ngumu kwa upande wa ccm.

Prof Safari alisema katika shauri hatoweza kusimamia badala yake atakuwa mshauri mkuu kwa mawakili watakao pewa kazi hiyo sababu kuu inayo mfanya ashindwe kusikiliza nikuwa kazi nyingi zimembana.

Akitoa angalizo kwa chama hicho kuwa baadhi ya kesi zitafunguliwa katika mahakama hiyo kutokana na jaji aliyekuwa akisimamia kutotoa ufafanuzi zaidi kama tuhuma nyingine ikiwa na ile ya rushwa ya mwigulu mchemba.


CHADEMA wilaya.

Mwenyekiti wa chama chadema wilaya Hamis Majimoto alikikupokea taarifa hiyo na kusema kuwa chama hicho kimejipanga vilivyo kuhakikisha haki itatendeka katika mahakama ya rufaa.

Alisema kuwa kwa kushirikiana na mawakili wa awari wa kesi hiyo chama hicho pamoja na mlalamika kashindye cha hakitomtupa kwa hatua aliyofikia hivi sasa.

Alikishutumu ccm kwa kufanya ucheleweshaji wa uchaguzi mdogo jimboni hapa hasa kwa kukimbilia mahakama ya rufaa.

‘’Ccm wanafanya janja ya mahakamani lakini ukweli wa kesi hii wanaujua vizuri wanawa nyima haki wananchi wa Igunga’’alisema majimoto.

 KAFUMU.

Aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo Dk,Kafumu alipoulizwa kuhusu taarifa hizi alikili kuwepo kwa taarifa hizo lakini alisema kuwa suala hilo limewasilishwa na watu wa chama wilaya.
Kafumu alisema kuwa hata saini hajaweka na kuongeza chama wanalishugulikia.

''miminafahamu kuhusu hilo lakini lipo mikononi mwachama hata saini sijaweka nadhani wao watakuwa na majibu zaidi nafahamu kinachoendelea''alisema kafumu.



Kashindye

Joseph kashindye alipoulizwa juu ya kusudio hilo alikili kupata taarifa hizo na kusema kwa mahakama hiyo ya rufaa itatoa haki kwa wanyonge.

Kashindye aliendelea kusema kuwa taarifa hizo amezipata kutoka kwa katibu wa chama wilaya kuwa ccm wametoa kusudio la rufaa.

Alisema kuwa chama hicho kimejipanga kukabiliana na chama ccm mpaka mwisho wa maamuzi wa mahakama hiyo ufike.

Aliongeza kuwa katika rufaa hiyo mawakili ambao walisimamia kesi hiyo wataendelea nayo mpaka mwisho kwani wao ndio wanafahamu ugumu wa kesi hiyo na urahisi wake.

mwisho.

No comments:

Post a Comment