Thursday, September 6, 2012

WALALAMIKIA KUUZIWA HOSPITALI YA WILAYA YA NZEGA

Na Lucas Raphael,Nzega
walamikia kuuziwa kwa Damu hospitali ya wilaya ya Nzega

BAADHI ya wananchi Wilayani Nzega Mkoani Tabora wamewalalamikia baadhi ya wahudumu wa Kitengo cha Maabara katika Hospitali ya wilaya ya Nzega kwa kujihusisha na biashara haramu ya kuuza Damu.

Wakizungumza na waandishi wa habari kwa nyakatati tofauti wananchi hao walisema kuwa baadhi ya watumishi wa kitengo hicho cha maabara wanajihusisha uuzaji wa damu pindi wangonjwa wanapo hitaji huduma hiyo.

Walisema kuwa kitendo cha kuuza dama ni kinyume na taratibu za utendaji wa kazi hiyo na kuongeza kuwa baadhi ya watu hushindwa kumudu gharama hizo na kupelekea kuhatarisha maisha ya watu na wengine kupoteza maisha yao kutokana na biashara hiyo haramu.

Taarifa hizi za biashara haramu ya damu zimekuwa zikilalamikiwa na wananchi kwa muda mrefu lakini hakuna hatua zinazo chukuliwa mpaka kupelekea wagonjwa kadhaa kupoteza maisha kutokana na upungufu wa dama wakati huo huduma hiyo ipo hospitalini hapo.

Wameziomba taasisi mbalimbali ikiwepo na takukuru kuchunguza kwa umakini tatizo hilo ilikukomesha Biashara hiyo haramu ya damu ikiwa na kuchukua maamuzi magumu ya kuwafikisha mahakamani watuhumiwa watakao bain ika.

‘’Mimi nilikuwa na dada yangu anajifungua bahati mbaya alitoka damu sana tukaambiwa anahitaji damu lakini tulijitokeza wengi kupima tukaambiwa damu zetu haziko sawa na ya mgonjwa wakasema kuna mtu anajitolea kutoa damu lakini mpatie chochote hali hiyo iliendelea mpaka dada yangu alipoteza maisha’’alisema mmoja ya wananchi jina lake limehifadhiwa.

Waliongeza kuwa damu hiyo huuzwa kuanzia shilingi 50,000 mpaka 40,000 na zaidi ya bei hizo kutokana na mteja atakae jitokeza.


Kisasu Sikalwanda ni katibu wa hospitali hiyo ya wilaya alipoulizwa kuhusu tuhuma hizo alikiri kuwepo kwa malalamiko hayo ya wananchi kuuziwa damu na kudai kuwa kitendo cha kuuza damu ni kosa katika idara hiyo.

Alisema tayari hatua za awali zimechukuliwa na kupelekwa ngazi za juu za uongozi zinaendelea kufanyiwa kazi na kuongeza kuwa damu katika hospitali hiyo ipo kwa sasa na kuwataka wananchi hao kutoa ushirikiano katika uongozi husika.

Aliwataka watumishi wa kitengo hicho cha maabala na watumishi wengine wafuate taratibu na maadili ya utendaji kazi sambamba na kuachana na vitendo hivyo haramu.

Sikalwanda alisema kuwa wananchi wanapaswa kutoa taarifa mapema kwa uongozi na hatua kari zitachukuliwa aliongeza kuwa taasisi mbalimbali ikiwepona takukuru ziwasaidie wananchi hao kukomesha vitendo hivyo vichafu katika Hospitali hiyo ya wilaya.

Mwisho.

No comments:

Post a Comment