Sunday, September 9, 2012

MDAHALO WA KATIBA MPYA



Na Lucas Raphael,Tabora
Mdahalo Katiba.
Wananchi wa kata ya Igalula Wilaya ya Uyui mkoaniTabora wamesema kwamba katiba mpya ya Tanzania iwe na kipengele kinachowakataza viongozi kwenda kutibiwa njue ya nchi na baadala yake watibile humu humu nchi.
Lengo la viongozi hauo kutibiwa humu nchi ni kuhakikisha huduma nzuri za matibabu zinatolewa kwa wananchi wote na sio kwa kundi moja la watu wachache .
 Hayo waliyaeleza kwenye mdahalo wa kuwahamasisha wananchi kujitokeza kutoa mawazo na michango yao katika mchakato wa kuunda katiba mpya pindi tume ya kukusanya maoni itakapopita kijijini hapo kwa ajili ya kazi hiyo.
Akizungumza katika kijiji cha Igulalu kaya ya Igalula mmoja wa washiriki wa mdahalo huo ,Maneno Keye alisema huduma za Afya sio nzuri kwa sasa kwani wananchi wanapata dawa ambazo muda wake umeshakkwisha .
Alisema kwamba kiti cha dawa kinacholetwa katika zahanati hakuna dawa bora ambazo zinazoweza kuwatib wananchi kwa kipindi hicho ,ndio hata Hospital za Rufaa pia hakuna huduma bora zinaweza kuwafanya viongozi kutibiwa huko .
Keye aliendelea kusema kwamba hali hiyo ya huduma mbovu za hospital zetu ndio maana viongozi mbalimbalui wanakimbilia kutibiwa nje ya nchi na kuziacha hospital zetu hazina madawa ya kutofa hata vifaa vya kuwez kuwatibu watanzania.
“katibu ikatanze viongozi kwenda kutibiwa huko nje kwa kufanya hivyo serikali itaboresha miundombinu ya hospital zetu kwani matibabu huyo yanawahusu watanzania wote “alisema keye.
Hata hivyo alisema kwamba iwapo zahanati hospital na zile za Rufaa zitakuwa na vifaa vya kutosha na waatalaam wazuri katika fani hiyo ya tiba hakika hakuna kiongozi ambaye hatakwenda kutibiwa huko nje ya nchi.
Aidha madam Hadija Shoo alisema kwamba  katiba mpya ijali usawa wa kijinsia kwani wanawake wengi wa vijiji wamekuwa kama ni watumwa kwa waume zao kwani waliowengi wanaolewa kama wafanyakzi wa ndani na sio wake kwa upendo hakuna.
Awali mwezeshaji wa mdahalo huo ,Christopher Nyamwanji aliwataka wananchi wa Igalula kushiriki kikamilifu kutoa mawazo na michango yao katika mchakato wa uundwaji wa katiba mpya wakati tume ya kukusanya maoni kwa wananchi itakapopita kwa ajili kufanya kazi hiyo.
Alisema kwamba iwapo kila mwananchi atatoa maoni kikamilifu na kupendekeza kuwa katiba ijayo iwe na muundo upi, hakika matukio kama.  ambayo yamekuwa yakijitokeza hivi sasa hapa nchini
Nae Mwenyekiti Shirika la Mtandao wa Maendeleo ya wananchi wilaya ya Uyui (UCODEN) ambao ndio waandaaji wa Mdahalo huo, Ally Magoha alisema kuwa katiba ni wananchi, mafanikio na machungu ya watanzania, hivyo ni muhimu kwa kila mmoja kutoa mchango na mawazo yake katika mchakato wa kuunda katiba mpya ili kuweza kupata katiba ambayo itakidhi matakwa ya umma wa watanzania.
UCODEN ni Shirika lisilo la kiserikali ambalo limekuwa likijishughulisha na kazi za maendeleo wilaya ya Uyui mkoani Tabora ambapo kwa mujibu wa Magoha wanatarajia kufanya midahalo kama hiyo katika vijiji vya Bukumbi, Ilolangulu na Kizengi, na kwamba lengo kuu la kufanyika kwa midahalo hiyo ni kutoa uamsho kwa wananchi kuhusu mambo mbalimbali ikiwemo suala la katiba.
Mdahalo huo ulioendeshwa na shirika lisilo kuwa la kiserikali la UCODEN na kufadhili na foundation For Civil Society.

Mwisho




No comments:

Post a Comment