Tuesday, September 11, 2012

Na:Robert Kakwesi,Tabora
Mtu mmoja amefariki dunia na wengine zaidi ya kumi kujeruhiwa baada ya basi walilokuwa 
wakisafiria kupinduka wilayani uyui.

 
Akizungumza kwa niaba ya kamanda wa polisi mkoani Tabora,Anthony Ruta,Mrakibu mwandamizi wa polisi,John Kauga, amesema ajali hiyo imetokea eneo la kizengi wilayani uyui baada ya basi la kampuni ya Muro kupinduka.





Kauga amesema mwanamke mmoja amefariki duniua katika ajali hiyo ambaye bado hajatambulika na mwili wake umehifadhiwa
 chumba cha maiti cha hospitali ya mkoa,kitete.

majeruhi zaidi ya kumi wamelazwa katika Hospitali hiyo huku Daktari wa Mkoa,Leslie Mhina,akisema majeruhi wanazidfi kuongezeka.

akizungumzia chanzo cha ajali hiyo,mrakibu mwandamizi Kauga amesema ni baada ya dereva wa basi hilo lenye namba za usajili T 904 BWA
,Sihaba Mohamed kumuachia utingo wake ambaye jina lake halijapatikana kuendesha basi hilo na kusababisha ajali.

Amesema dereva na utingo wake wote wamekimbia baada ya ajali iliyotokea jana usiku jumanne majira ya saa tatu kasorobo na wanatafutwa.

No comments:

Post a Comment