Tuesday, September 4, 2012

UKARABATI WA RELI




Naibu waziri wa uchukuzi Dkt Charles Tizeba ameitaka kampuni ya china ya CCECC EAST AFRICHA LTD kukamilisha kubalilisha reli kwa mujibu wa mkataba wao unavyosema ili kuruhusu shirika hilo la kufanya kazi zake kwa ufanisi zaidi .

Waziri huyo aliyasema hayo wakati wa ziara yake katika reli ya kati aliyoifanya jana akiwa pamoja na viongozi waandamizi wa shirika hilo kukangua mradi wa kubadilisha reli ya kati  kutoka yenye uzito mwepesi na kuweka yenye uzito wa kila 40 kwa mita moja kwa ajili ya kuwezesha reli hiyo kuweza kupitika kwa urahisi tofauti na ilivyosasa .

Mradi huo wa kubadilisha reli  wenye urefu wa kilometa 89 kutoka sheshini ya Kitalaka hadi eneo la Malongwe utakao gharimu jumla ya fedha za kitanzania shilingi bilioni 29. kwa kipindi cha mwaka mmoja

Akizungumza na meneja mradi wa kampuni hiyo ya kichina CCECC WU ZEGANG ,alimwambia kuwa wahakikishe kuwa muda uliowekwa ndio muda huo huo wanakabidhi mradi huyo na taratibu zote ziwe zimekwisha kulingana na mkataba wa mwaka mmoja .

“Mkataba wenu na serikali ya Tanzania kupitia rahco uwe umekamilika kwa muda uleule ambao mlisaini kwa ajili ya kumilisha kazi iliyopo mbele yenu ambayo imeanza toka septemba 1 mwaka huu”alisema Dkt Tizeba.

Naibu waziri huyo alisema kwamba kubadilishwa kwa reli hiyo kutalisaidia shirika la Reli hapa Nchini litakuwa linafanya kazi kwa  ufanisi zaidi wa kuweza kupitisha mizigo mizito tofauri na sasa .

Aidha alisema matatizo yaliyopo sasa ya reli nyembamba inasababisha reli kuhama hama na kupatab ajali za mara kwa mara  ikiwe na mzigo mkubwa hayo yote hayatakuwepo tena bali itabaki kwenye madaraja ambayo nayo yatafanyiwa matengenzo kuruhusu kupitisha mizigo mizito.

Dkt Tizeba alisema kwamba mradi huo ni ukamilishaji wa kilometa 197 ambazo zilikuwa zikifanyiwa marekebisho ya kuweka reli zinazoweza kupitsha mabehewa yenye na mizigo mizito  .

Hata hivyo alisema kwamba reli yetu sio mbaya sana kiasi kwamba ni mbovu kila eneo na kuna maeneo mengine yamefanyiwa kazi na mengine pia yanahitaji matengenezo.

Kaimu meneja mradi huo kutoka RAHCO, Mahizo Mgenzi alisema kukamilisha kwa matengenezo hayo kutakuwa kumeboresha miundombimu ya shirika la Reli na sehemu inayafanyiwa ukarabati itaweza kupisha treni kwa kasi zaidi na mizigo yenye uzito mkubwa.

Alisema kwamba kukamilika kwa reli hiyo usalama wa reli ,mabahewa ya aina yote na yatakuwa kwenye usalama zaidi tofauti na sasa ambavyo mabehewa yanayumbayumba na kusababisha abiri kuwa na hofu mara wanaposafiri.

Mwisho

No comments:

Post a Comment