Monday, September 10, 2012

MWIGULU MCHEMBA AIPASHA CHADEMA.

MWIGULU  MCHEMBA AIPASHA CHADEMA.

Na,LUCAS RAPHAEL IGUNGA

MWEKAHIZINA wa chama cha mapinduzi ccm taifa ,Mbunge wa jimbo la Iramba Maghalibi Mwigulu Mchemba  amesema kuwa chama cha Demokrasia na maendeleo chadema kina weka chuki kwa wananchi wa Tanzania na pamoja na kusababisha mauaji ya raia wema.

Alisema hayo jana katika mkutano wa chama cha mapinduzi(CCM) uliofanyika katika viwanja vya sokoine wilayani Igunga kuwa chadema wanasababisha mauaji ya raia  kwa masirahi yao huku akitolea mifano ya mikoa ya Arusha,Morogoro pamoja na jimboni kwake Iramba Maghalibi.

Alisema chadema kinafanya kazi kupandikiza chuki kwa wananchi kwa kutumia mikutano yao ikiwa na mauaji kila kielekeapo chama hicho pamoja na kukazana kulituhumu jeshi la polis kuhusika na mauaji hayo.

’’chadema wanaeneza mauaji kasha wanawasingizia polis lakini mauaji hayo yote yana sababishwa na chadema hivyo wananchi waogopeni hawa ni mashetani’’alisema Mbunge huyo.

Alieleza kuwa chadema hawafurahii maendeleo ya wananchi kwa kile walicho kifanya cha kukata rufaa katika ubunge wa Dkt,Kafumu kwa kushinikiza malalamiko yasiyo ya msingi.

Alisema hoja zilizo pelekwa na chadema katika mahakama kuu ya kanda ikiwa ni pamoja na ugawaji wa mahindi,ahadi za daraja la mbuntu,kutoa kauli ya bakwata na hoja yingine zilizo somwa na mahakama hiyo sio za msingi kutengua jimbo hilo ambapo shuguli za ugawaji mahindi na mambo mengine ya kiserikali yalikuwa yakiendelea kama kawaida kwa nyakati mbalimbali.

Alisema wananchi wa Igunga walikuwa na njaa hivyo serikali iliweza kupeleka misaada hiyo kwa wananchi wake pamoja na kutekeleza ahadi yake ambaqyo ilikuwepo katika irani ya chama hicho cha ujenzi wa daraja la mbutu.

Mwigulu alisema kuwa wapinzani wote hawajapata sera mbadala ya kuwa ongoza wananchi hivyo bado hawana uwezo wa kuweza kuongoza nchi hii.

Aliongeza kuwa Jaji aliye toahukumu hiyo ya Dkt,Kafumu  anakaa kijiji kimoja na mwenyekiti wa chadema Freemani Mbowe hivyo ilikuwa lazima jaji huyo awasaidie katika kesi hiyo.

Ambapo jaji aliye kuwa akiendesha kesi hiyo ni Jaji Mery Nsimbo shangali

‘’Jaji huyo aliye amua toa hukumu hiyo anakaa kijiji kimoja na mwenyekiti wa chadema mbowe hivyo lazima awapendelee katika maamuzi hayo ili mahusiano yawe mazuri zaidi’’alisema.

Alisema viongozi wa chadema hawana upeo zaidi wa kuona mbali hasa kwa kushangilia mambo yasiyo ya msingi ikiwa ni pamoja na kutuhumu rais kikwete kwa kuendekeza suala la dini.

Alisema hata kama uchaguzi mdogo ukifanyika jimboni Igunga ccm itashinda kwa kishindo kutokana na chama hicho kuweka mizizi sehemu mbalimbali za jimbo hilo.

‘’Iwe usiku,mchana,mashariki,maghalibi,kazikasini,kusini lazima ccm itashinda kwani jimbo hilo nilakwetu lazima tushende’’alisema mchemba.

Akiwa hakikishia siku chache zijazo chama hicho kitakata rufaa katika mahakama kuu ya rufaa kwa kutumia hoja mbandala ambazo zilizo chambuliwa na wana sheria wa chama hicho.

Alisema hoja hizo nitofauti na zile alizo kuwa akidai katibu mkuu wa chadema Dkt, slaa kuwa ccm haina uwezo wa kukata rufaa hiyo kutokana na hoja zilizo mbele ya mahakama ya rufaa.

Vyanzo vya habari kutoka ndani ya ccm vilidai kuwa chama hicho kimefanya mkutano huo kutokana na chadema kufanya mkutano katika eneo hilo kwa kutoa maneno juu ya m aamuzi ya mahakama hiyo.

’’Lengo ni kujibu hoja za chadema hivyo ndio maana tumeamua na sisi tufanye mkutano huo ilituwe wazito hapa mjini igunga’’kilisema chanzo hicho.

Awari ya hapo katibu Mkuu wa chama cha Demokrasia na Maendeleo(chadema) Dkt,Willbrod slaa akiwa katika viwanja hivyo vya sokoine wiki chache zilizo pita alikitahadhalisha chama cha mapinduzi kukata rufaa kisije kika umbuka katika mahakama ya rufaa.

Akitoa mifano mbalimbli ya rushwa zilizo fanyWa na chama cha mapinduzi CCM na mweka hazina wa chama cha mapinduzi ccm mwigulu mchemba kutoa rushwa katika sehemu mbalimbali katika jimbo hilo.

Alisema kuwa chama hicho kimejipanga kukabiliana na rufaa hiyo na kuahidi kuwa rufaa hiyo itakuwa ya aina yake kwani chama hicho kitafungua kesi nyingine juu ya vigogo wa chama hicho katika uchaguzi huo mdogo.

Katibu huyo aliwashutum mwekahazi wa chama cha mapinduzi ccm,kutoa Rushwa,katibu Mkuu wa chama cha mapinduzi ccm Willson Mukama kudai kuwa chadema ilileta makondo pamoja na waziri wa Ujenzi Pombe Magufuli kutoa ahadi za ujenzi wa Daraja la mbuntu pamoja na ahadi ya kugawa mahindi.

MWIsHO.


No comments:

Post a Comment