Saturday, November 3, 2012

IGP MWEMA AFANYA MABADILIKO KWA BAADHI YA MAKAMANDA WA MIKOA NA VIKOSI

 

Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Said Mwema (pichani), amefanya mabadiliko kwa baadhi ya makamanda wa Polisi wa mikoa na vikosi.

Mabadiliko hayo ni pamoja na aliyekuwa kamanda wa
Polisi mkoa wa Pwani SACP Ernest Mangu anayekwenda kuwa Kamanda wa Polisi Mkoa
wa Mwanza kuziba pengo la marehemu ACP Liberatus
Barlow, 

ACP David Misime aliyekuwa
kamanda wa Polisi mkoa wa Temeke kwenda kuwa Kamanda wa Polisi mkoa wa Dodoma kuchukua nafasi ya SACP Zelothe Steven anayestaafu. Vilevile, aliyekuwa kamanda wa Polisi Viwanja vya Ndege ACP Ulrich Matei anakwenda kuwa kamanda wa Polisi mkoa wa Pwani.


Aidha, wengine ni kutoka Makao Makuu ya Polisi na Makao Makuu Idara ya Upelelezi ambapo ACP Engelbert Kiondo kutoka makao makuu Idara ya Upelelezi  anakwenda kuwa kamanda wa Polisi mkoa wa Temeke, ACP Rashid Seif kutoka Makao Makuu ya Polisi Kwenda kuwa Kamanda wa kikosi cha Tazara, ACP Deusdedit Kato kutoka Makao Makuu ya
Polisi kwenda kuwa Kamanda wa Polisi Viwanja vya Ndege, ACP Shaban Hiki kutoka Kamanda wa Kikosi cha Ufundi kwenda Makao Makuu ya Polisi na ACP Lucas Mkondya kutoka Makao Makuu ya Polisi kwenda kuwa Kamanda wa Kikosi cha Ufundi.

Mabadiliko hayo pia yamehusisha aliyekuwa Afisa Mnadhimu
wa kikosi  cha Usalama Barabarani  ACP Johansen Kahatano anayekwenda kusimamia  Mradi wa SMARTER Traffic ambapo nafasi yake itachukuliwa na aliyekuwa RTO mkoa wa Pwani ACP Swalehe Mbaga. 

Uhamisho huo pia umewahusisha baadhi ya Wakuu wa Operesheni wa Mikoa, Wakuu wa Vikosi vya Kutuliza Ghasia vya Mikoa, Wakuu wa Polisi wa Wilaya na Wakuu wa Upelelezi wa Wilaya. Uhamisho huo ni wa kawaida kwa mujibu wa kanuni, taratibu na miongozo ya Jeshi la Polisi.

Imetolewa na:

 Advera
Senso-ASP

 Msemaji wa
Jeshi la Polisi (T).

No comments:

Post a Comment