Na Lucas Raphael,Tabora
Wananchi
wa kata ya Nkiniziwa na kata ya Ndala wilayani Nzega Mkoani Tabora wamesema
katiba itakayo patikana itambue uhuru wa vyombo vya Habari.
Wakizungumza
kwa nyakati tofauti wakati wakitoa maoni ya kupata katiba mpya mbele ya tume ya
mabadiliko ya katiba ilipo watembelea wananchi hao walisema kuwa uhuru wa
vyombo vya habari utambulike ili wananchi wapate habari .
Walisema
kuwa vyombo vya habari vitambulike vipewe uhuru zaidi wa kutoa habari sehemu
yeyote ya idara bila kupewa vizuizi kwa idara yeyote ili kupata habari za
ukakika.
Walisema
kuwa baadhi ya vyombo vya habari vinafungiwa kwa kuandika habari za uhakika za
kuhusu vigogo wa serikali hali ambayo wananchi wanashindwa kupata habari
kutokana na vizuizi vinavyo wekwa.
Walisema
kuwa habari ni mmoja ya mawasiliano ya muhimu baina ya serikali na wananchi
hivyo vyombo vya habari view huru kuandika habari yeyote lakini visivunje
sheria.
Wakitoa
maelekezo katika katiba hiyo waitakayo walisema vyombo vya habari vizibitiwe
viwe vichache na vifunguliwe kwa mpango maalumu tofauti na sasa vyombo hivyo ni
vingi ambavyo havina wataalam wa kuviongoza.
Waliongeza
kuwa katiba hiyo iwatambue waandishi wa Habari kwa kuwalinda katika mikutano na
mihadhara mbalimbali kwan I watu hao wanalitumikia taifa kwa kutoa taalifa
ikiwa na kuweka sheria kwa vyombo vya habari kmuwapatia uwezo zaidi wa kufanya
kazi.
Walisema
kuwa waandishi wa Habari hawawezeshwi na vyombo vyao hivyo katiba ijayo iweke
sheria ya kuvibana vyombo hivyo kuwawezesha waandishi wake ilikupata habari
zenye uhakika zaidi.
Mwisho.
No comments:
Post a Comment