Msanii wa muziki wa kizazi kipya (Bongo flava) na Balozi wa Airttel Tanzania, Ambwene Yessaya 'AY'
Msanii
wa muziki wa kizazi kipya (Bongo flava) na Balozi wa Ambwene Yessaya
'AY' akiwashukuru watanzania kwa kumpigia kura na kumwezesha kupata tuzo
hiyo kulia ni Afisa Uhusiano wa Airtel Jane Matinde na kushoto ni DJ
wake Athur Baraka.
Afisa Uhusiano
wa Airtel Jane Matinde akiongea wakati wa mkutano na waandishi wa habari
ambapo Airtel imempongeza AY balozi wake kwa kupata tuzo ya chanel O ya
video bora, Katikati ni AY akifatiwa na DJ wake Athur Baraka
====== ======== ==========
Airtel Tanzania yaanda Part ya kumpongeza Balozi wake AY Nyumbani Lounge
Kampuni
ya simu za mkononi ya Airtel wakiwa na balozi wake Ambwene Yessaya “AY”
leo wamewashukuru watanzania kwa kumpigia kura msaani maarufu wa kizazi
kipya Ambwene Yessaya “ AY “ na kumwezesha kuibuka mshindi wa tuzo ya kwanza katika kipengele cha Most Gifted East African video of the Year kupitia kibao chake kipya kijulikanacho kama “ I don’t wanna be alone”
Akiongea na
wandishi wa habari katika Ofisi za Airtel leo AY amechukua fulsa
kuwashukuru watanzania kwa kumpigia kura na kuweza kumwezesha kuibuka na
ushindi. Aidha alivishukuru vyombo vya habari kwa kuendelea
kushirikiana naye katika kufikisha habari na kumsaidia kupata tuzo hiyo.
Naye Afisa
uhusino wa Airtel Jane Matinde alisema” tunafurahi kuona msanii AY
ambaye ni balozi wetu kuibuka na tuzo iliyoshirikisha wasanii mbalimbali
toka Afrika, sisi tunasikia furaha kuona mafanikio ya wasanii wetu
nchini yakiendelea kukua na ndio sababu leo tuko hapa kusherehekea
ushindi huu kwa pamoja na kuwashukuru watanzania kwa kumuwezesha AY
kupata tuzo hii kwa kura zenu.
Tunapenda pia
kuchukua fulsa hii kuwaalika watanzani na wateja wetu leo pale nyumbani
lounge usiku kuanzi saa tatu tuweze kujumuika na AY na kumpongeza kupata
tuzo hii. Tutakuwa na wasanii wengi pamoja na wadau mbalimbali wa
Musiki na pia utapata muda kupiga picha na msanii huyo na Tuzo yake.
No comments:
Post a Comment