BENKI YA NMB YACHANGIA MILIONI 30 KUFANIKISHA UZINDUZI WA MKOA WA KATAVI

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania Mh. Mizengo Pinda akipokea mfano wa hundi ya shilingi
milioni 15 kutoka kwa Robert Pascal Mkuu wa Kitengo cha Kilimo benki ya
NMB, kama mchango wa benki hiyo kwa ajili ya kununulia madawati ya
shule za msingi katika mkoa huo, Ikiwa ni mchango wa benki hiyo katika
maendeleo ya elimu Mkoani Katavi, ambao umezinduliwa rasmi na Makamu wa
Rais Dkt. Mohamed Gharib Bilal kwenye viwanja vya Kashaulili mjini
Mpanda, na kuhudhuriwa na wananchi wengi wa mkoa huo. Mbali
na fedha hizo benki ya NMB pia imetoa kiasi cha shilingi milioni 15
zingine na vifaa vya michezo ikiwemo mipira na jezi kwa ajili ya timu za
mpira wa miguu za mkoa wa Rukwa na Katavi kwa ajili ya kufanikisha
mchezo wa mpira wa miguu kati ya timu hizo wakati wa uzinduzi katika
mkoa huo , pamoja na maandalizi mengine ya shughuli za uzinduzi, jumla
ya fedha iliyotolewa na Benki ya NMB ni shilingi milioni 30 za
Kitanzania.
Makamu
wa Rais Dkt. Mohamed Gharib Bilal akizungumza na wafanyakazi wa benki
ya NMB wakati alipotembelea banda la benki hiyo katika maonyesho
yaliyofanyika wakati wa uzinduzi wa mkoa mpya wa Katavi mjini Mpanda.
Makamu
wa Rais Dkt. Mohamed Gharib Bilal (kushoto) akiteta jambo na Waziri
Mkuu,Mh. Mizengo Pinda, wakati wa kutathmini mrejesho wa kongamano la
Uwekezaji katika Ukanda wa Ziwa Tanganyika uliofanyika Oktoba 17 mwaka
jana mjini Mpanda.
Mkuu
wa mkoa wa Katavi Dkt Rajab Rutengwe akikaribisha wageni mbalimbali
waliofika kwa ajili ya uzinduzi wa Kongamano hilo na Mkoa wa Katavi
lililofanyika kwenye ukumbi wa Idara ya Maji Mjini Mpanda hivi karibuni.
Waziri
Mkuu,Mh. Mizengo Pinda akimshukuru mama Domina Ferouz Mkuu wa Biashara
kati ya benki ya NMB na Serikali, mara baada ya kupokea hundi hiyo
wakati wa uzinduzi rasmi wa mkoa wa Katavi, katikati ni Lucrencia
Makinya Meneja wa Kanda ya Nyanda za juu Kusini NMB.
Wananchi
wakitembelea moja ya Banda ya wawekezaji wa kigeni wakati wa maonyesho
hayo ya uzinduzi wa mkoa wa Katavi uliofanyika leo mjini Mpanda.
Mkuu
wa Wilaya ya Mpanda Bw. Paza Mwamlima akitoa utaratibu wakati wa
Kongamano la Tathmini ya Mkutano wa Uwekezaji Ukanda wa Ziwa Tanganyika
lililofanyika sambamba na uzinduzi wa mkoa wa Katavi kuanzia juzi na
kumalizika jana mjini Mpanda huku uzinduzi wa mkoa huo ukifanyika leo.
Baadhi ya maofisa mbalimbali wa Serikali waliohudhuria katika Kongamano hilo lililofanyika mjini Mpanda mkoa mpya wa Katavi.
Mabalozi
kutoka nchi mbalimbali walihudhuria kongamano hilo zikiwemo Burundi,
Misri Zambia, Japan na DRC Congo hapa wakifuatilia Mada katika
kongamano hilo.
Mkuu
wa mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya akikaribishwa na Lucrencia
Makinya Meneja wa Kanda ya Nyanda za juu Kusini Benki ya NMB, katika
chakula cha jioni kilichoandaliwa na benki ya NMB kwa ajili ya wakuu wa
mikoa na wakuu wa wilaya kwenye hoteli ya Lyamba lya Mfipa mjini Mpanda
Wafanyakazi
wa benki ya NMB wakijumuika katika picha ya pamoja mara baada ya kula
Chakula cha jioni na wakuu wa Mikoa na wilaya kwenye hoteli ya Lyamba
Lya Mfipa mjini Mpanda.
Maofisa
mbalimbali wa benki ya NMB kutoka makao makuu , Mbeya na Mpanda
wakiwa katika picha ya pamoja wakati benki hiyo ilipoandaa chakula cha
jioni kwa wakuu wa Mikoa na Wilaya kwenye hoteli ya Lyamba Lya Mfipa
mjini Mpanda jana
No comments:
Post a Comment