Thursday, November 22, 2012

MAZISHI YA ALIYEKUWA MKURUGENZI WA ORION TABORA HOTEL KUFANYIKA LEO


Aliyekuwa mkurugenzi wa Orion Tabora Hotel,Poley Ahmed enzi za uhai wake katika kuchangia shughuli mbalimbali za Kijamii. 



Habari  kutoka kwa jamaa  wa karibu wa marehemu mkurugenzi huyo Poley Ahmed aliyefariki dunia siku ya Jumanne saa moja usiku baada ya kuugua kwa muda mrefu....,Mazishi yake yanatarajiwa kufanyika hapo kesho baada ya kuwasili ndugu na jamaa kutoka nje ya nchi na wale walioko nje ya mkoa wa Tabora.

Hata hivyo kumekuwa na taarifa ya mwili wa marehemu Poley kuzikwa makaburi ya Isevya Quater manispaa ya Tabora mahali ambako baadhi ya marehemu nduguze walizikwa hapo lakini kumeingia utata kwakuwa eneo hilo liliwahi kupigwa marufuku shughuli za mazishi na uongozi wa halmashauri ya manispaa ya Tabora.

Marehemu Poley Ahmed ambaye amefariki akiwa na umri wa miaka 53,maelfu ya watu kutoka Tabora na nje ya mkoa wanatarajiwa kushiriki katika kumsindikiza mpendwa wao kwenye safari yake ya mwisho.

  TABORALEOHABARI inaungana na familia ya marehemu Poley Ahmed katika kipindi hiki kigumu cha msiba wa mpendwa wetu,.....MUNGU AIPUMZISHE ROHO YA MAREHEMU POLEY AHMED PEPONI AMIN....  

No comments:

Post a Comment