Friday, November 16, 2012

KATIBU MKUU WA WIZARA YA HABARI AFANYA ZIARA BARAZA LA KISWAHILI LEO



Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bwana Seith Kamuhanda akikagua moja ya majengo ya Baraza la Kiswahili Tanzania (BAKITA) alipofanya ziara ya ukaguzi wa Ofisi hizo mpya zilizopo Kijitonyama Jijini Dar es Salaam.Anaemuelekeza kushoto ni Mtendaji Mkuu wa Bakita Dkt. Selemani Sewangi. 
Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bwana Seith Kamuhanda akiongea na watumishi wa Baraza la Kiswahili Tanzania (hawapo pichani) alipofanya ziara ya ukaguzi wa Ofisi hizo mpya zilizopo maeneo ya Kijitonyama Jijini Dar es Salaam.Kushoto ni Mtendaji Mkuu wa BAKITA Dkt. Seleman Sewangi  na kulia ni Mkurugenzi wa Maendeleo ya Utamaduni Profesa Hermas Mwansoko.
Baadhi ya watumishi wa Baraza la Kiswahili Tanzania (BAKITA) wakimsikiliza Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo (hayupo pichani) alipofanya ziara ya ukaguzi wa Ofisi hizo mpya zilizopo Kijitonyama Jijini Dar es Salaam. Picha na Benjamin Sawe wa WHVUM.

No comments:

Post a Comment