Thursday, November 22, 2012

Ndege Insurance Brokers yasherehekea miaka yake 45,yazindua nembo yake mpya ya kibiashara



Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Bima ya Ndege Dkt. Sebastian Ndege akimkabidhi Mgeni rasmi Kamishna wa Mamlaka ya Usimamizi wa Shughuli za Bima nchini (TIRA) Bw. Israel Kamuzora tuzo ya heshima kubwa kwa kutoa mchango mkubwa  kwa namna moja ama nyingine katika kampuni hiyo ya Ndege Insurance,hafla hiyo imefanyika usiku wa kuamkia leo ndani ya hotel ya Serena,jijini Dar.
Mfanyakazi Bora wa Mwaka wa kampuni ya Ngede Insurance Brokers Bw. Haruna Said akikabidhiwa tuzo yake na Mgeni rasmi Bw. Israel Kamuzora sambamba..
Mwanasheria wa kampuni ya Ndege Insurance Brokers Bw. Justin Ndege akikabidhi tuzo kwa mfanyakazi aliyedumu muda mrefu katika kampuni hiyo Bi. Eutrophia Benedict (kushoto). Wanaoshuhudia tukio hilo ni mgeni rasmi na Dkt. Sebastian Ndege.
Kamishna wa Mamlaka ya Usimamizi wa Shughuli za Bima nchini (TIRA) Bw. Israel Kamuzora akizungumza machache mbele ya wageni waalikwa mbalimbali (hawapo pichani) waliofika kwenye maadhimisho ya kutimiza miaka 45 tangu kuanzishwa kwake ikiwemo sambamba na kuzindua nembo yake mpya ya Ndege Insurance Brokers.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa kampuni hiyo Bi. Renatha Mushi akimlisha keki Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Bima ya Ndege Dkt. Sebastian Ndege

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa kampuni hiyo Bi. Renatha Mushi akindaa keki ya kulimsha Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Bima ya Ndege Dkt. Sebastian Ndege
Mgeni rasmi Bw. Israel Kamuzora (katikati) wakikata keki na Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Bima ya Ndege Dkt. Sebastian Ndege (kulia) pamoja Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa kampuni hiyo Bi. Renatha Mushi Ndege ikiwa ni maaadhimisho ya miaka 45 ya tangu kuanzishwa kwake kutoa Huduma za Bima nchini.
Makofi baada ya keki kukatwa


Kamishna wa Mamlaka ya Usimamizi wa Shughuli za Bima nchini (TIRA) Bw. Israel Kamuzora akizindua nembo mpya ya Ndege Insurance Brokers kwenye hafla ya kutimiza miaka 45 ya kampuni hiyo. Anayeshuhudia ni Afisa Mtendaji Mkuu wa kampuni hiyo Dkt. Sebastian Ndege.
 SKYLIGHT BAND ikota burudani kusindikiza maadhimisho ya miaka 45 ya Ndege Insurance Brokers tangu kuanzishwa kwake.
Wanahabari wakiwa bize kuchukua tukio la kukatwa kwa keki

Mmoja wa waimbaji wa bendi ya Skylight akiimba jukwaani wakati wa hiyo ilipokuwa ikiendelea.
Wadau waliokuwepo kwenye hafla hiyo iliyofana kwa kiasi kikubwa.
Wadau mbalimbali wakishuhudia tukio adhimu la mafanikio makubwa ya Ndege Insurance Brokers kwenye 
Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Bima ya Ndege Dkt. Sebastian Ndege akizungumza wakati wa hafla ya maadhimisho ya miaka 45 ya Kampuni hiyo tangu kuanzishwa kwake, iliyofanyika usiku wa kuamkia leo katika Hoteli ya  Serena jijini Dar es Salaam.
Wadau mbalimbali waliohudhuria hafla Ndege Insurance Brokers  


Pichani juu na chini ni baadhi ya wadau wakijadiliana hapa na pale wakati wa hafla ya Ndege Insurance Brokers. 
Pichani shoto ni Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Bima ya Ndege Dkt. Sebastian Ndege akiwa katika picha ya pamoja na wadau mbalimbali wa kampuni yake ya  Ndege Insurance Brokers kwenye 
Wadau wakijadiliana jambo wakati wa hafla ya Ndege Insurance Brokers kwenye iliofanyika ndani ya hoteli ya Serena,usiku wa kuamkia leo jijini Dar

No comments:

Post a Comment