Monday, November 26, 2012

RAIS KIKWETE AMUAPISHA KATIBU WA TUME YA KUREKEBISHA SHERIA

 Rais Jakaya Kikwete akimuapisha Katibu wa Tume ya Kurekebisha Sheria, Winfrida Korosso mara baada ikulu jijini Dar es Salaam, leo. (Picha na Habari Mseto Blog)
Rais Jakaya Kikwete akimkabidhi  vitendea kazi Katibu wa Tume ya Kurekebisha Sheria, Winfrida Korosso mara baada ya kuapishwa kuwa katibu wa tume hiyo, Ikulu,  jijini Dar es Salaam. 
Rais Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na wanafamilia
(Picha na Habari Mseto Blog)
DAR ES SALAAM, Tanzania

RAIS Jakaya Kikwete, leo amewaapisha majaji wa mahakama kuu ya rufani, wajumbe wa tume ya uchaguzi na katibu wa tume ya kurekebisha sheria, hafla iliyofanyika katika makazi ya Rais Ikulu jijini Dar esSalaam.

Majaji walioapishwa  kufanya kazi katika mahakama ya rufani ni Bethel Makani na Ibrahim Khamis Jumaa,wakati Jaji mstaafu John Mkwawa ameapishwa kuwa mjumbe wa tume ya taifa ya uchaguzi, huku Winnfrida Koroso, akiapishwa kuwa mjumbe wa tume ya kurekebisha sheria.

Wakizungumza baada ya kuapishwa kushika nafasi hizo wateule hao walisema watahakikisha wanafanya kazi kwa uadilifu na moyo wa kujitolea kuhakikisha haki inatendeka katika nafasi walizo nazo.

Makani alisema katika nafasi yake hiyo mpya anayoenda kufanyia kazi kuna changamoto nyingi ikiwemo wananchi kudhani suala la kucheleweshwa au kuahirishwa kwa kesi mbalimbali kunasababishwa na mahakimu pamoja na majaji.

“Ni mara chache hakimu kuahirisha kesi kama kutakuwa kila kitu kimekamilika nah ii hali ya kuchelewa kwa kesi ina mzunguko mkubwa ikiwa ni pamoja na wananchi wenyewe kusdhindwa kutoa ushirikiano na idara husikia katika kupata ukweli wa kufanyia uamuzi”alisema Makani.

Kwaq Upande wake jaji John Mkwawa alisema katika nafasi anayoenda kuhudumu changamoto zilizopo ni pamoja na kufanyia marekebisho daftari la kudumu la wapiga kura iuli liendane na mahitaji ya sasa ya watanzania.

Alisema changamoto nyingine ni ucheleweshaji wa matokeo baada ya uchaguzi na kwamba hali hiyo inatokana na kutokuwepo kwa teknolijia ya kisasa ya kuweza kufanyia kazi hiyo.

No comments:

Post a Comment