Friday, November 16, 2012

SERENGETI BOYS KUSHINDA NYUMBANI KWANZA


Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kusaidia timu ya Serengeti Boys ishinde Bw. Kassim Dewji akizungumza na waandishi wa habari kwenye hoteli ya JB Belmont jana wakati akielezea mikakati ya kamati hiyo katika kuhamasisha wadau ili waweze kujitolea na kuhakikisha timu hiyo inashinda mchezo wa nyumbani kabla ya marudiano ili kujihakikishia kufuzu michuano ya Kombe la Afrika kwa vijana litakalofanyika nchini Moroco Mwezi Machi mwakani, Kulia ni mjumbe wa kamati hiyo Bw Salim na katikati ni Katibu Mkuu wa Shirikisho la mpira wa miguu nchini Tanzania TFF Bw. Angetile Osiah Jumla ya shilingi milioni 35 zimepatikana ambapo zitasaidia mambo mbalimbali ya maandalizi ya mchezo wa timu ya Serengeti Boys na Congo Brazaville utakaofanyika siku ya jumapili Novemba 17.
Katibu Mkuu wa Shirikisho la mpira wa miguu nchini Tanzania TFF Bw. Angetile Osiah akizungumza katika mkutano huo kulia ni Henry Tandau katibu mkuu wa kamati hiyo na katikati ni Kassim Dewji makamu mwenyekiti wa kamati
Waandishi wa habari wakifuatilia taarifa iliyokuwa ikitolewa na makamu mwenyekiti wa kamati ya kusaidia ushindi wa timu ya taifa ya vijana Serengeti Boys.

No comments:

Post a Comment