Monday, November 26, 2012

ZIARA YA KATIBU MKUU WA CCM ABDULRAHMAN KINANA MKOANI ARUSHA

Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akihutubia maelfu ya wananchi katika  mkutano wa hadhara uliofanyika jana kwenye Uwanja  wa Sheikh Amri Abeid mjini Arusha leo (Picha na Bashir Nkoromo)
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape akisalimiana na Lowassa Uwanja wa Ndege wa Arusha. Kushoto Katibu wa CCM mkoa wa Arusha Mary Chatanda
Pikipiki zikiongoza msafara wa Kinana, kutoka Uwanja wa Ndege wa Arusha
Kinana akifungua shina la wakereketwa wajasiriamali wa CCM la Nguruma, Arumeru, Arusha
Kikundi cha Ngoma ya Kimasai kikitumuiza katika  mkutano wa Meru, Arusha
Kinana akisalimia wananchi baada ya kuwasili uwanja wa Usa River kuhutubia mkutano wa hadhara
Nape akizungumza jambo la Lowassa kwenye mkutano wa Kinana uliofanyika Usa River, Arusha
Wazee wa Kimeru, wakimkabidhi vitendea kazi vya jadi, Katibu Mkuu wa CCM, Kinana katika mkutano uliofanyika Usa River, Arusha. Anayemkabidhi ni Ezrom Sumari.
Kinana akiwa na zana za jadi alizokabidhiwa kwa heshima yake na wazee wa Meru, katika Mkutano wa CCM uliofanyika Usa River, Arusha

 
Mzee Wilson Meng’atu akimvisha vazi la heshima Nape Nnauye kama ishara ya wazee wa Kimeru kutambua upambanaji wake katika kujenga Chama, wakati wa mkutano wa Usa River, Arusha
 
Wazee wa Kimeru wakimvisha Wasira vazi la jadi kuheshimu mapambano yake katika ujenzi wa Chama

No comments:

Post a Comment