Thursday, November 22, 2012

WAISLAM TABORA WAANDAMANA,POLISI WAWAPA ULINZI WA KUTOSHA


 Baadhi ya Waislamu mjini Tabora wakifanya maandamano ya amani kuadhimisha mwaka mpya wa kiislam  1434 Hijiria huku makachero wa Jeshi la Polisi wakiwapatia ulinzi wa kutosha.
 Sheikh wa wilaya ya Tabora mjini Ustaadh Ramadhan Rashid bin Jumaa akiwaasa waislamu waliokuwa wamehudhuria katika maandamano hayo.
Umati mkubwa wa waislamu wake kwa waume wakiwa wanawasikiliza viongozi wao mara baada ya kukamilisha maandamano hayo yaliyopewa ulinzi wa kutosha kutoka Jeshi la Polisi Tabora.
 Ustaadh Ali Kondera ambaye ni mjumbe wa Baraza la Maimamu mkoani Tabora akizungumza na waislamu kwa niaba ya Sheikh mkuu wa mkoa wa Tabora ambapo aliwaasa waislamu kuimarisha amani na utulivu uliopo nchini.

No comments:

Post a Comment