Thursday, November 22, 2012

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AFUNGUA MAADHIMISHO YA SIKU YA TAKWIMU AFRIKA, LEO DAR


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akihutubia wananchi  wakati wa ufunguzi wa  Maadhimisho ya Siku ya Takwimu Afrika, yaliyofanyika kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam, leo.
 Baadhi ya wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Kisutu ya Jijini Dar es Salaam, wakiwa katika maadhimisho hayo, wakimsikiliza Makamu wa Rais, Dkt. Bilal.
 Sehemu ya wananchi waliohudhuria maadhimisho hayo kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja leo.
 Wanafunzi wa Chuo Kikuu, wakiigiza kuhusu malengo ya Maadhimisho hayo na maana ya Takwimu.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Viongozi wa Ofisi ya Takwimu waliokuwa Meza Kuu, baada ya kufungua rasmi Maadhimisho hayo leo.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Wanafunzi wa Vyuo Vikuu waliohudhuria ufunguzi wa maadhimisho hayo baada ya ufunguzi rasmi uliofanyika kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja, jijini Dar es Salaam leo.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Wanafunzi wa Shule za Sekondari, waliohudhuria ufunguzi wa maadhimisho hayo baada ya ufunguzi rasmi uliofanyika kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja, jijini Dar es Salaam leo.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Mkurugenzi wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu, Brandina Chuwa, wakati alipokuwa akiwasili kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam, leo kwa ajili ya kufungua rasmi Maadhimisho ya Siku ya Takwimu Afrika. 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na Kamishna wa Sensa , Hajjat Amina Mrisho Said, wakati akiondoka katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam, leo baada ya kufungua rasmi Maadhimisho ya Siku ya Takwimu Afrika.

No comments:

Post a Comment