Thursday, November 15, 2012

SERENGETI WAZINDUA KINYWAJI KISICHO NA KILEVI ALVARO


Mmoja kati ya vijana akicheza”Break Dance”wakati wa uzinduzi rasmi wa kinywaji kipya kisichokuwa na kilevi cha Alvaro kinachotengenezwa na Kampuni ya bia ya Serengeti Breweries LTD.



Baadhi ya vijana walioshiriki katika uzinduzi wa kinywaji kisichokuwa na kilevi cha Alvaro  kinachotengenezwa na Kampuni ya bia ya Serengeti Breweries wakionesha umahiri wao wa kucheza katika uzinduzi rasmi wa kinywaji hicho jijini Dar es Salaam hapo jana.
Warembo walioshiriki katika uzinduzi rasmi wa kinywaji kipya kisichokuwa na kilevi cha aina ya Alvaro kinachotengenezwa na Kampuni ya bia ya Serengeti Breweries LTD,Wakionesha umahiri wao wa kucheza katika uzinduzi huo uliofanyika jijini Dar es Salaam.
Vijana walioshiriki katika uzinduzi wa kinywaji kisichokuwa na kilevi cha Alvaro kinachotengenezwa na Kampuni ya bia ya Serengeti Breweries,wakigonganisha chupa zao kuashiria ishara ya uzinduzi rasmi wa kinywaji hicho hapo jana jijini Da es Salaam.
---

NA MWANDISHI WETU
KAMPUNI ya Bia ya Serengeti imezindua kinywaji kipya kisicho na kilevi kinachoitwa Alvaro ambacho kimekuwa kikizalishwa muda mrefu katika nchi nyingine za Afrika Mashariki.
Katika uzinduzi wa aina yake uliofanyika mwishoni mwa wiki jijin Dar es Salaam, Meneja wa Kinywaji hicho Anita Msangi alisema kinywaji hicho kitakidhi wateja wanaotumia vinywaji visivyo na kilevi
Uzinduzi wa kinywaji hicho uliofanyika katika kumbi za Mlimani City na Quality Plaza jijini, Dar es Salaam, ulivutia watu kutoka matabaka mbalimbali ambao walionekana kufuruhishwa na ladha ya kinywaji hicho.
Akizungumza katika sherehe hizo, Bw. Njowoka aliahidi watumiaji wa kinywaji hicho na vingine vinavyotengezwa na kampuni ya Serengeti kuwa kampuni yake imejipanga kuona kuwa wateja wanapata bidhaa bora zenye viwango vya hali ya juu vinavyostahili na kukidhi matakwa ya wateja wake.
Pamoja na wageni wengi waliofika kwenye uzinduzi huo, sherehe za kuzindua kinywaji hicho pia zilipambwa na vikundi mbalimbali vya vijana ambavyo vilionesha uweso mkubwa katika sanaa ya muziki pamoja na kucheza dansi.
Kinywaji cha Alvaro kimekua kikizalishwa kwa muda mrefu katika nchi za Uganda na Kenya kupitia kampuni mama ya kiwanda cha kutengzeneza bia cha Serengeti iitwayo East African Breweries Limited.

No comments:

Post a Comment