Tuesday, November 13, 2012

AIRTEL DIVA WATOA MSAADA KWA WODI YA WATOTO WANAOUNGUA MARADHI YA KANSA HOSPITAL YA TAIFA YA MUHIMBILI




Mkurugenzi wa Mawasaliano wa Airtel bi Beatrice Singano  Mallya(kulia)  akikabidhi  computer kwa  Mkuu wa kitengo cha wodi ya watoto wanaougua Saratani  kwa Daktari Sulende Kubhodja  wa  hospitali ya Muhimbili , (kati ni) meneja wa jengo la wodi hiyo sista Judica  Mwambo. Wafanyakazi wanawake wa Airtel Tanzania  walitembelea hospitalini hapo  mwishoni mwa wiki hii na kujitolea pia vifaa mbalimbali vikiwemo vitendea kazi vitakavyotumika kafanya usafi kwa wagonjwa  waliolazwa hospitalini hapo Muhimbili
Wafanyakazi wanawake wa Airtel (Airtel Divas) wakikaribishwa na Meneja wa wodi ya watoto wanaougua Saratani katika Hospitali ya Muhimbili sista Judica Mwambo ambapo hao walitembelea hospitalini hapo  mwishoni mwa wiki hii na kujitolea pia vifaa mbalimbali vikiwemo vitendea kazi vitakavyotumika kafanya usafi kwa wagonjwa  waliolazwa hospitalini hapo Muhimbili
 Mkurugenzi wa Mawasaliano wa Airtel bi Beatrice Singano Mallya (wapili kulia)akiongea na mmoja wa watoto  waiolazwa katika hospitali ya Muhimbili mwishoni mwa wiki hii ambapo wafanyakazi  wanawake wa Airtel waliamua kutembea watoto wenye kuugua Saratani katika Hospitali hiyo mwishoni mwa wiki hii, akifuwatiwa na Afisa uhusiano wa Airtel Tanzania Jane Matinde. Airtel ilijitolea vitu mbalimabli kwaajili ya hospitali hiyo ikiwemo computer, pamoja sabuni, miswaki, na dawa za meno kwaajili ya wagonjwa hao.

Wafanyakazi wanawake wa Airtel (Airtel Divas) wakiingia na mizigo yao katika wodi wa wagonjwa wanasumbuliwa na maradhi ya  Saratani katika Hospitali ya Muhimbili, wafanyakazi hao walitembelea hospitalini hapo mwishoni mwa wiki hii na kujitolea pia vifaa mbalimbali vikiwemo vitendea kazi vitakavyotumika kafanya usafi kwa wagonjwa  waliolazwa hospitalini hapo Muhimbili
Wafanyakazi wanawake wa Airtel Tanzania wakiwa katika picha ya pamoja na watoto wanaogua Saratani katika wodi ya Muhimbili walipowatembelea mwishoni mwa wiki hii ambapo Airtel walitoa misaada mbalimbali ikiwepo  komputa , sabuni, dawa za mswaki na mahitaji mengine muhimu.

No comments:

Post a Comment