Tuesday, November 13, 2012

WASHINDI 66 WAPATIKANA KWENYE DROOO YA KWANZA YA KI-COLLEGE ZAIDI NA NMB


Meneja Huduma kwa wateja wa benki ya NMB Tawi la Bank House Steven Chavala (mwenye Suti Nyeusi) akibonyeza kitufe kuwapata washindi wa promosheni ya Ki-College zaidi na NMB. Kutoka (kushoto) ni Meneja Amana wa NMB, Boma Raballa, Meneja Masoko wa NMB, Shilla Senkoro na Mkaguzi wa bodi ya michezo ya kubahatisha ya Taifa, Humud Abdulhussein na Meneja bidhaa wa selcom, Julio Batalio.
 Meneja Masoko wa NMB, Shilla Senkoro akionesha zawadi ya taa ya kutumia mionzi ya jua 
 Meneja wa Huduma kwa Wateja wa Benki ya NMB, Stephen Chavallah akibonyeza kitufe cha kompyuta kuwatafuta washindi wa promosheni hiyo.
 Meneja wa Huduma kwa Wateja wa Benki ya NMB, Stephen Chavallah (wa pili kulia) akiangalia namna washindi wa promosheni ya Ki-College Zaidi na NMB wanavyopatikana wakati wa droo ya kwanza iliyochezeshwa Makao Makuu ya benki hiyo jijini Dar es Salaam jana. Kulia ni Mkaguzi wa Michezo ya Kubahatisha, Humudi Abdulhussein. Kushoto ni Meneja wa Amana, Boma Raballa na Meneja Masoko, Shilla Senkoro
..........................
Octoba 1, 2012 NMB ilizindua promosheni ya Ki-COLLEGE zaidi na NMB inayowawezesha wanafunzi wenye akaunti ya NMB Student Account kupata nafasi ya kuingia kwenye droo na kujishindia zawadi mbalimbali kama: iPad, Samsung Galaxy, Amana maradufu, flash disk, fulana za NMB, taa inayotumia mionzi ya jua. Hivyo basi, wanafunzi waliofungua NMB Student Account, walioweka amana katika akaunti zao au kujiungana NMB mobile wameweza kuingia kwenye droo na wamepata nafasi ya kujishindia zawadi kwenye promosheni ya Ki COLLEGE zaidi na NMB.

Katika droo ya kwanza ya Ki COLLEGE zaidi na NMB iliyochezeshwa tarehe 12 Novemba, 2012, jumla ya washindi 66 walijishindia zawadi mbalimbali kama ifuatavyo; Ipad 2, Samsung Galaxy 2, Amana maradufu 2, taa inayotumia mionzi ya jua na jezi za timu ya Taifa 30.

Pamoja na kampeni hii, wanafunzi walioshinda na watakao fungua NMB Student Account wataendelea kufurahia huduma za NMB Student Account kama: Kufungua akaunti kwa Sh. 10,000 tu (pamoja na NMB ATM kadi),kujiunga na huduma ya NMB mobile bure kupata huduma ya ujumbe mfupi kila utoapo fedha kwenye ATM ya NMB bure, kuchukua fedha hadi Sh.1,000,000 kwenye NMB ATM kwa siku na kupata huduma kupitia matawi zaidi ya 143 na NMB ATM zaidi ya 450 nchi nzima.

Ili uweze kuingia kwenye droo na kupata nafasi ya kujishindia zawadi kwenye promosheni ya Ki COLLEGE zaidi na NMB, fungua NMB Student Account, weka amana katika akaunti yako, tumia au jiunge na NMB mobile .Ikiwa hujatumia akaunti yako kawa muda mrefu tembelea tawi la NMB ili nawe ushiriki katika promosheni hii ya ki-COLLEGE zaidi na NMB inayoendelea hadi Desemba 31, 2012.

No comments:

Post a Comment