Monday, December 10, 2012

MAKAMU WA RAISI DK BILAL KATIKA SHEREHE ZA UTOAJI WA NISHANI

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimpongeza mwanamuziki wa Msondo, Muhidin Gurumo, kwa kutunukiwa Nishani ya sanaa na Rais Kikwete.
 Rais Jakaya, na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, Rais wa Zanzibar, Dkt. Shein na mkewe, Bi Mwanamwema, wakiwa katika picha ya pamoja na wasanii wa kikundi cha sanaa cha Taifa cha Rwanda wakati wa hafla ya usiku ya miaka 51 ya Uhuru, iliyofanyika kwenye Viwanja vya Ikulu, jijini Dar es Salaam jana.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiteta jambo na Mwenyekiti wa NCCR Mageuzi, James Mbatia, wakati wa sherehe ya maadhimisho ya miaka 51 ya Uhuru iliyofanyika kwenye Viwanja vya Ikulu Dar jana usiku.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiteta jambo na Inspekta General, Said Mwema na Kamishna wa Polisi Zanzibar, Mussa Ali, wakati wa sherehe ya maadhimisho ya miaka 51 ya Uhuru iliyofanyika kwenye Viwanja vya Ikulu Dar jana usiku.

No comments:

Post a Comment