Sunday, December 23, 2012

UHALIFU WAWATESA WAKAZI WA ISEVYA MANISPAA YA TABORA


 Mama mmoja mkazi wa Isevya akitoa machozi kwa uchungu na kushindwa kutoa maelezo jinsi alivyofanyiwa vitendo vya kiharifu na baadhi ya vijana wa Isevya ambao wamekuwa wakijihusisha na vitendo wizi na ujambazi,ilikuwa ni mkutano wa pamoja kati ya wakazi wa kata hiyo uongozi wa Jeshi la Polisi mkoa wa Tabora.
 Mkuu wa upelelezi makosa ya jinai mkoa wa Tabora RCO BUKOMBE akizungumza na wananchi wa kata ya Isevya manispaa ya Tabora katika mkutano wa hadhara uliofanyika kituo kidogo cha Polisi Isevya.
 Mkuu wa kituo kikubwa cha Polisi Tabora anayeshughulikia kitengo cha Polisi Jamii Joseph Matui akitoa maelezo ya dhana shirikishi jamii kwa wakazi wa kata ya Isevya manispaa ya Tabora baada ya kuitishwa kwa kikao ambacho wakazi hao walikuwa wakifikisha malalamiko yao kuhusu mgambo wanaofanya kazi katika kituo hicho Kidogo cha Polisi Isevya,ambapo imeelezwa kuwa mgambo hao wamekuwa wakiomba na kupokea rushwa kwa wananchi na kusababisha kero kubwa.

No comments:

Post a Comment