Monday, December 10, 2012

TRENI YA MWAKYEMBE YAPOKELEWA KWA SHANGWE MWANZA

 


Wananchi wa Mwanza wakiipokea treni ya Shirika la Reli Tanzania(TRL), kwa ujumbe wa Mabango wakatii treni hiyo ilipowasili Mkoani Hap oleo mchana. Treni hiyo ilisitisha huduma zake tangu Mwaka 2009, Imeanza safari zake rasmi kwa mabehewa Sita, likiwemo moja la daraja la Kwanza. Treni hiyo itakuwa ikifanya safari zake Mara mbili kwa Wiki.

Baadhi ya Abiria wa wanaotumia usafiri wa Treni ya Shirika la reli Tanzania (TRL), waliotokea jijini Dar es Salaam ijumaa kuelekea Mkoani Mwanza wakiwa ndani ya behewa la Daraja la Tatu kama walivyokutwa leo asubuhi .Treni hiyo imeanza safari zake kutokea Dar kwenda Mwanza.
Naibu Waziri wa Uchukuzi, Dkt. Charles Tizeba(mwenye suti Nyeusi),akiwa ndani ya Mabehewa ya Treni ya Shirika la Reli Tanzania(TRL)leo Asubuhi wakati alipoipokea treni hiyo iliyokuwa ikitokea jijini Dar es Slaam.Treni hiyo ya kwenda Mwanza imeanza rasmi Ijumaa kutokea Dar kwenda Mwanza baada ya kusitisha huduma zake tangu mwaka 2009.
Wananchi wa Mkoani Mwanza wakipunga mkono kuashiria furaha yao kwa kuanza kwa Safari za Treni ya Shirika la Reli Tanzania (TRL).Treni hiyo imeanza safari zake ijumaa kwa kutokea Dar es Salaam kuja Mwanza.
Baadhi ya Abiria wanaotumia usafiri wa Treni ya Shirika La Reli Tanzania(TRL),wakishuka katika Stesheni ya Mwanza Leo Mchana kutokea dare s Salaam.treni ilisitisha safari zake kwenda Mwanza mwaka 2009 na Ijumaa ilianza safari kutokea Dar kwenda Mwanza.
Naibu Waziri wa Uchukuzi, Dkt Charles Tizeba, akisisitiza wafanya biashara waliojenga vibanda na kufanyia biashara karibu na Miundombinu ya Reli katika eneo la stesheni ya Reli Mwanza mpaka Maeneo ya Mamlaka ya Bandari(TPA),kuhama katika maeneo hayo kama Sheria ya Reli inavyoelekeza.Picha Kwa hisani ya Michuzi Blog

No comments:

Post a Comment