Sunday, December 23, 2012

UVCCM TABORA WADONDOSHA MACHOZI HADHARANI


 Baadhi ya makada wa Uvccm manispaa ya Tabora wamejikuta wakibubujikwa na machozi wakati wakiangalia igizo lililobeba hisia kali dhidi ya manyanyaso kwa watoto yatima wanayofanyiwa na watu wanaochukua dhamana ya kuwalea.Igizo ambalo lilioneshwa na kikundi cha Nuru cha mjini Tabora.
 Mtoto Maria Ramadhani(Baby)akionesha hisia kali wakati wa moja ya Igizo lililowagusa idadi kubwa ya watu wakati wa maonesho ya uzinduzi wa kikundi chake cha Nuru Art Group & House of Talent kata ya Ng'ambo manispaa ya Tabora ambapo katika onesho hilo baadhi ya viongozi wa CCM wilaya ya Tabora walihudhuria wakiongozwa na Meya wa Manispaa ya Tabora Bw.Ghulam Dewij.
 Kutoka kushoto ni Meya wa Manispaa ya Tabora Bw.Ghulam Dewij,Mwenyekiti wa ccm wilaya ya Tabora Bw.Moshi Nkonkota na Mwenyekiti wa Uvccm wilaya ya Tabora Mwl.Lucas nao waliguswa na ujumbe katika Igizo hilo la mateso kwa watoto yatima.
Mwenyekiti wa UWT wilaya ya Tabora  Bi.Joyce akiwa na huzuni katika onesho hilo lililofanyika soko la Ng'ambo manispaa ya Tabora.

No comments:

Post a Comment