Tuesday, December 25, 2012

mipasho leo Vegetable Garden Pub ya Ilala, Dar

Gwiji la Muziki wa Taarabu nchini, na Mshindi wa Tuzo ya Mtumbuizaji bora wa Kike, Hadija Kopa akifanya makamuzi  katika tamasha maalum la Washindi wa Kili Music Award 2012 kwenye uwanja wa Ushirika Moshi Mkoani Kilimanjaro

Na Peter Mwenda

MALKIA wa Mipasho nchini, Khadija Omar Kopa na kundi lake la  Tanzania One Theatre (TOT) leo kitatoa shoo kabambe kusherekea sikukuu ya Krismas kwa wakazi wa Kata ya Kivule, Ilala, jijini Dar es salaam kusherekea sikukuu ya Krismas kwenye ukumbi wa Vegetable Garden Pub.

Akizungumza jana, Kopa alisema kikundi hicho ambacho kinatamba na nyimbo kemkem za taarab zinazotingisha katika miondoko ya Pwani ukiwemo Full Stop, Stop in Town na Mjini Chuo Kikuu ameahidi kukonga nyoyo za mashabiki wake katika eneo hilo kwenye sikukuu hiyo.

Alisema TOT taarab imesheheni kila idara ikiwa na wanamuziki wenye uwezo mkubwa wa kupiga taarab yenye mahadhi yanayokubalika akiwepo mkongwe Abdul Misambano, Mwanamtama Amir, Ali Star, Rukia Juma na Kopa Junior anayeimba nyimbo za Omar Kopa.

Mkurugenzi wa Vegetable Garden Pub, Anicety Mkwaya alisema maandalizi ya burudani hiyo imekamilika na zawadi zitatolewa kwa wale watakaocheza taarab vizuri na watakaovaa vizuri.

Alisema burudani katika ukumbi huo zinaendelea ambapo Januari 29, 2013  bendi ya Msondo Ngoma itatoa burudani katika ukumbi huo.

No comments:

Post a Comment