Sunday, December 23, 2012

YUSUPH KITUMBO ATANGAZWA MWENYEKITI MPYA WA TAREFA


Mwenyekiti wa kamati ya uchaguzi wa chama cha mpira wa miguu mkioa wa Tabora Tarefa Mkama Bwire akitangaza matokeo ya uchaguzi huo ambapo amemtangaza Yusuph Kitumbo kuwa Mwenyekiti wa Tarefa kwa kupata kura 16 kati ya kura halali 24,nafasi ya pili imeshikwa na Mussa Ntimizi ambaye amepata kura 8 huku Laurent Paul akiwa ameambulia patupu.

Aidha matokeo hayo ya uchaguzi Fath Dewij ameshinda nafasi ya katibu wa Tarefa kwa kumshinda Albert Sitta ambaye alikuwa akitetea nafasi yake aliyoiongoza kwa muda mrefu.

Hata hivyo msimamizi huyo wa uchaguzi Bwire mkama amesema bado kuna nafasi ambazo hazikufanyiwa uchaguzi kwa kile alichodai kuwa ni kukosa wagombea na kuachwa wazi huku akizitaja kuwa ni nafasi ya Katibu msaidizi na Mwekahazina.

No comments:

Post a Comment