Tuesday, December 4, 2012

MWENYEKITI WA CCM NZEGA AWATAKA WANANCHI KULIMA MAZAO YANAYO HIMILI UKAME



NA LUCAS RAPHAEL,TABORA


Wananchi wa wilaya ya  Nzega mkoani Tabora wametakiwa kulima mazao yanayohimili ukame kutokana na mvua za masika zinazoendelea kunyesha kutotosheleza kwa mazao mengine ambayo hulimwa kila mwaka hasa mahindi .  
Wito huo umetolewa na Mwenyekiti wa chama cha mapinduzi CCM wilaya Amosi Kanuda katika kikao cha wanachama wa chama hicho kilichofanyika katika Jimbo la Bukene wilayani hapa. 

Kanuda alisema wananchi wahamasishwe kulima mazao ya yanayohimili ukame kutokana na mvua za msimu huu kutotosheleza zaidi kwa mazao mengine ambayo wamezoea kulimwa na wananchi wengi wa wilaya hiyo.  

Alisema baadhi ya wananchi hulima mazao kwa mazoea ,hali ambayo hugeuka kuwa ombaomba kila mwaka wa chakula cha njaa kutokana na kutopokea ushauri huo wa kitaalamu kutokana na eneo hili la wilaya ya nzega . 

Akitoa maelekezo kwa wanachama hao kuwa mazao wanayo takiwa kulimwa na wananchi wa wilaya hiyo ni pamoja na mtama,viazi vitam,mihogo pamoja na mazao ya kibiashara ambayo yanayo himili ukame ikiwa na pamba na Alizeti.  

Mwenyekiti akiendelea kutoa wito wake alisema wananchi wakipokea kauli hiyo na kulima mazao hayo hawatakuwa ombamba wa chakula kila mwaka kutokana na kupata mazao mengi ikiwa na kupata mazao mengi ya kibiashara kwani mazao hayo yote yanahimili ukame.  

Aliongeza kuwa chama hicho kitaishauri serikali ya wilaya kuhakikisha mbegu za mtama na mbegu za mazao mengine zinaletwa mapema ili wananchi waendelee na kilimo hicho waendane na kalenda ya kilimo. 

Mwenyekiti huyo aliwataka wananchi kutunza chakula walicho nacho kwa matumizi mazuri ambayo amchokitawasaidi kuwafikisha msimu wa mavuno utakao kuja. 

’’wananchi na wanachama chama hakijawakataza kulima mahindi mpunga hapana lakini nguvu kubwa wekene kwenye mazao yanayo himili ukame kwani mvua hizi hazitoshi,tusilime kwa mazoea kama tulivyo zoea tunataka tuondokane na kuwa ombaomba’’alisema mwenyekiti huyo.  

Kwaupande wake katibu wa chama hicho wilaya, Kajoro Vyohoroka aliwataka wananchi kuitikia wito huo kwa pamoja bila kujali itikadi ya vyama vya siasa,dini wala kabila kutokana na suala hilo kumgusa kila mtu.  

Alisema endapo wananchi wataitikia wito huo wataondokana na kuwa ombaomba wakila mwaka wa chakula cha msaada nabadala yake itakuwa historia kwa wananchi hao. 

Kwa upande wa wananchama hao na wananchi waliobahatika kuzungumza na mara baada ya kikoa hicho  walisema kuwa serikali ipeleke haraka mbegu hizo mtama ikiwa na mihogo ili wananchi waweze kulima mapema zao hilo .
 
Mwisho.


No comments:

Post a Comment