Sunday, December 16, 2012

MRADI WA VIJIJIN VYA MILENIA MBOLA

KATIBU TAWALA WA MKOA WA TABORA KUDRA MWNYIMVUA WAKITETA JAMBO NA VIONGOZI WA VIJIJI VYA MILENIA DR GEORGE SEMPEHO NA MWENYEKITI WA HALASHAURI YA WILAYA YA UYUI SAID NTAHODI NA DR NYANZI

DR  GEORGE SEMPEHO AKITOA MAELEZO KABLA MGENI RASMI HAJAFUNGUA MKUTANO HUO WA WADAU WA VIJIJI VYA MELINIA KATIKA UKUMBI WA MTEMI ISKE MWANAKINYUNGI

VIONGOZI WA CHAMA NA SERIKALI  MKONI TABORA WAKIONGOZWA NA MKUU WA WILAYA YA UYUI LUCY MAHENGA

KATIBU TAWALA MKOA WA TABORA KUDRA MWINYIMVUA AKIFUNGUA MKUTANO WA SIKU MBILI WA WADAU WA VIJIJI VYA MILENIA MBOLA MVP


Na Lucas Raphael,Tabora

Milenia

Mradi wa Kijiji cha millennia – Mbola  unatarajia kuhitimishwa rasmi mwaka 2015 na hivyo kijiji hicho kitabaki kuwa kijiji cha mfano ambapo mbinu zilizotumika katika kuboresha maisha kwa wakazi wa kijiji hicho zitatumika kuendeleza vijiji vingine hapa nchini.

Akizungumza na kujadiliana na wadau kuhusu hali itakuwaje baada ya awamu ya pili ya mradi huo kukamilika ifikapo mwaka 2015, mkuu wa wilaya ya Uyui Mkoani Tabora, Lucy Mayenga, amesema serikali inajivunia uwepo wa mradi huo kwani ni kielelezo madhubuti cha maendeleo.

Alisema kuwa mradi huo umeweza kufanya mambo mengi ya maendeleo kwa wakazi wa kijiji cha millennia cha mbola mkoani Tabora, ambapo huduma za kijamii zinazotolewa katika kijiji hicho ni nzuri.

Alisema serikali na halmashauri zinapaswa kujifunza kupitia mradi huo, kwani imebainika kuwa mradi yote iliyotekelezwa katika kijiji hicho imejengwa kwa gharama nafuu huku miradi inayotekelezwa katika sehemu nyingine ikiwa na gharama kubwa.

Naye mratibu wa mradi wa vijiji vya milenia nchini, Dk. George Sempeho, amesema kwa kuwa mradi huo unafikia tamati hivi sasa, UNDP imeona itakuwa vyema kufanya tathmini na kuacha mradi huo ukiwa endelevu badala ya kuuacha holela na hatimae kufa.

Naye Mwenyekiti wa  halmashauri ya wilaya ya Uyui mkoani Tabora, Said Ntahondi, amesema kuwa kijiji hicho kimekuwa na maendeleo makubwa na kwamba mara zote mradi huo, umekuwa ukitumia njia shirikishi ambazo zimesaidia kufikiwa kwa maendeleo hayo.

Mwisho.

No comments:

Post a Comment