Sunday, December 23, 2012

MBUNGE MSTAAFU JIMBO LA TABORA MJINI AFARIKI GHAFLA


 
Marehemu Siraj Juma Kaboyonga aliyekuwa mbunge wa jimbo la Tabora mjini 2005 - 2010.

Mbunge mstaafu wa jimbo la Tabora mjini Mh.Siraj Kaboyonga amefariki dunia wakati akikimbizwa hospitali ya Muhimbili kufuatia kuugua ghafla shinikizo la damu majira ya saa tatu na nusu usiku wa kuamkia leo huko jijini Dar-es-salaam.

Taarifa kutoka kwa mtoto wa marehemu Kaboyonga,Bw.Juma Siraj ameuambia mtandao huu kuwa baba yake amefariki kifo cha ghafla wakati akiwa lango kuu la hospitali ya Muhimbili jijini Dar wakati alipopelekwa kwa ajili ya matibabu kufuatia ugonjwa wa ghafla uliompata kuanzia majira ya saa tatu usiku.

Bw.Juma amesema tayari mipango ya mazishi imekwisha kamilika na huenda akazikwa kesho majira ya saa saba mchana huko katika makaburi ya Kisutu jijini Dar ambapo kwasasa msiba upo eneo la Sinza Mori jirani na Charles Hilali.

INNALILLAH WAINAILLAIH RAJIUN  

No comments:

Post a Comment