Wednesday, December 5, 2012

Rais Kikwete afungua wodi ya Wazazi Hospitali ya Wazazi Kinyonga,Kilwa-Ahutubia mkutano wa Hadhara pia akagua Maabara katika Shule ya Sekondari Mitole


Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akifunua kitambaa katika jiwe la msingi wakati alipofungua rasmi Jengo la Wodi ya Wazazi katika Hospitali ya Kinyonga,wilayani Kilwa jana wakati wa kilele cha ziara yake ya siku tano ya kikazi Mkoani Lindi.Kulia aliyesimama ni Mganga mkuu wa Hospitali hiyo Dkt.Mike Mabimbi.
Mganga mkuu katika hospitali ya Kinyonga,wilayani Kilwa Dkt.Mike Mabimbi(kulia) akitoa maelezo kwa Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete muda mfupi baada ya Rais kufungua jengo la wazazi katika hospitali hiyo na kulikagua.Wodi hiyo ya Wazazi imejengwa ikiwa ni Mkakati wa kuboresha huduma ya Mama na mtoto Tanzania na ujenzi umefadhiliwa na Halmashauri ya Kilwa pamoja na Chama Cha Madaktari Bingwa wa Magonjwa ya akina mama Tanzania(AGOTA) na shirika la Uholanzi la Bioshape Benefit Foundation.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na baadhi ya wananchi waliohudhuria mkutano wa hadhara mjni Kilwa Kivinje,mkoani Lindi jana jioni.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwahutubia wananchi mjni Kilwa Kivinje jana jioni.Rais Kikwete aliyekuwa katika ziara ya kikazi ya siku tano Mkoani Lindi amerejea jijini Dar es Salaam jioni hii.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akingalia wanafunzi wakifanya majaribio ya kisayansi katika shule ya sekondari ya Mitole iliyopo wilayani Kilwa, wakati alipokuwa katika ziara ya kikazi Mkoani Lindi jana.Picha na Freddy Mar

No comments:

Post a Comment