Tuesday, December 4, 2012

WADAU WA UREMBO WASHINGTON DC USA, MAGGIE MUNTHALI ANAHAKI YA KUSHIRIKI KAMA MTANZANIA

Na Father Kidevu Blog, Dar Es Salaam


KAMATI ya Miss Tanzania imesema kuwa Mrembo Maggie Munthali hana pingamizi lolote katika kushiriki mashindano hayo kwa kutumia jina la Tanzania na badala yake kufanya hivyo anatumia uzalendo
wake kuitangaza nchi Kimataifa.


Ufafanuzi huo umekuja kufuatia malamiko yaliyotolewa na baadhi ya wadau wa Urembo hasa Watanzania waishio katika jiji la Washingtoni DC, Marekani juu ya Uhali wa Mrembo Maggie Munthali kuvaa beji ya Miss Tanzania katika mashindano ya kumsaka Miss Afrika USA 2012.

Akizungumza na Blogu hii Msemaji wa Kamati ya Miss Tanzania Hidan Ricco amesema kuwa Kamati ya Miss Tanzania haina kipingamizi chochote kwa mrembo huyo kushiriki mashindano hayo, kwani shindano hilo linawahusu warembo waishio huko lakini wanatoka Tanzania.

Awali akitoa historia ya Mrembo huyo, Rico alisema kuwa Kamati inamfahamu vyema mrembo Maggie Munthali kwani aliwahi kushiriki mashindano hayo ngazi ya Vitongoji na kuishia ngazi ya kanda.

Tumesoma maoni yenu kupitia mitandao ya kijamii Blogs inaohusu taarifa ya mrembo Maggie Munthali kushiriki shindano la urembo la Miss Africa USA.

“Mrembo Maggie Munthali alishiriki mashindano ya urembo ya Miss Tanzania Kitongoji cha MZIZIMA mwaka 2005.” Alisema Ricco.

Pia aliendelea kwa kusema kuwa Mrembo Maggie alikuwa miongoni wa waliofanikiwa kuingia TOP 3 ya shindano hilo hivyo kupata nafasi ya kuwakilisha kitongoji hicho katika ngazi ya KANDA YA ILALA  kwa mwaka huo.

Mrembo huyo hakupata nafasi  ya kuingia katika Fainali za Taifa kwa mwaka huo 2005. aliishia ngazi ya Kanda ya Ilala.

Kanda ya Ilala kwa mwaka huo iliwakilishwa na FEZA KESSY, Perminda Raj na LILIAN MUSHI, na mshindi wa mwaka huo alikuwa NANCY SUMARI ambaye pia alitwaa taji la MISS WORLD AFRICA 2005.
Ricco amesema Kamati ya Miss Tanzania haijui ni vigezo vipi vinatumika katika shindano hilo, na maamuzi yakumpa jina Miss Tanzania na Kamati inaamini kuwa ni mrembo anayewakilisha Tanzania  japokuwa hakuingia  katika Fainali za Taifa.

Kamati inamtakia kila la heri mrembo huyo na wengine watakaojitokeza kutangaza jina la Tanzania katika fani ya urembo.
 FatherKidevu Blog ilifanikiwa kufanya utafiti juu ya washiriki wa shindano  hilo na kubaini kuwa sio Mamiss halisi wa nchi walizotoka kwani baadhi  ya nchi walikuwa zaidi ya mmoja kama vile Kenya. 
Pia baadhi yao Umri unaonesha dhahiri kuwa umekwenda sana kwani washiriki  wanapoaswa kuana miaka kuanzia 18 lakini isizidi 29 na hawaendani na  vigezo halali vya mashindano ya Urembo yanayofanyika kila mwaka katika  nchi husika kwaajili ya kushiriki Miss World.

Haya ni baadhi ya Masharti na Vigezo vya Mshiriki ambayo yapo
katika mtandao huu   http://www.missafricaunitedstates.com/application/registration/

ELIGIBILITY

1.Applicant must have at least one parent from an African country.

2. An applicant with parents from two countries will choose to represent only one country of her choice.

3. Applicants must  be at least 18 years old on or before the date of the pageant she wishes to compete in.

4.Applicants above 29 years of age will not be accepted

5.We accept Applications from students, professionals and girls wishing to develop themselves and improve their status.

6. Applicants are strongly encouraged to have a humanitarian platform and realistic project to uplift the community in need.

7. No Pageant Experience is required.

8. Applicants must be female at birth and never married.

No comments:

Post a Comment