Saturday, December 1, 2012

CHADEMA YAMZOA MWENYEKITI WA UDP SIKONGE NA WENGINE 241


  



CHAMA cha Demokrasia na maendeleo CHADEMA,wilaya ya
Sikonge,kimeendelea kuitesa CCM kufuatia katibu wa chama cha UDP



wilaya hiyo Kazimoto Elias Kazimoto, kujiunga na chama hicho.

Kazimoto amehama na wanachama wa UDP,CUF na CCM 241 na kuhamia CHADEMA
akiwemo mwenyekiti wa wake Phillipo Elicado Kayumba ambapo Kazimoto
kwa sasa baada ya kuhama ni mwenyekiti wa kata ya Misheni na Kayumba
ni katibu mwenezi wa kata hiyo.

Aidha alisema baada ya kuhamia CHADEMA alikabidhiwa kadi namba CD 0559599.

Kazimoto alifafanua kuwa amejiunga na CHADEMA mapema mwezi agosti
20,2012 akiwa na idadi hiyo ya wananchama akidai hiyo ndiyo siri ya
CHADEMA kushinda kiti cha udiwani kata ya Ipole wilaya ya Sikonge.

Alisema kuwa baada ya kujiunga na CHADEMA sasa anajipanga kugombea
udiwani kata ya Misheni ambayo kwa sasa inashikiliwa na mwenyekiti wa
halmashauri ya wilaya hiyo Robert Kamoga (CCM).

Aliongeza kuwa baada ya kuhama na wanachama hao amejipanga kuhakikisha CHADEMA
kinakuwa na nguvu kubwa ili kushinda kiti cha ubunge na udiwani kwa
kata nyingin zaidi.

Aidha alisema kazi nyingine ni kuhakikisha CHADEMA kinakuwa na
wanachama waliohai wenye misimamo thabiti ili kukibeba chama.

Alisema siri ya ushindi na kupata idadi ya wananchama wengi kwa sasa
ndani ya CHADEMA kutasaidia chama chake kuimaliza CCM kwenye uchaguzi
hapo 2012.
“Wanacnchi waliowengi kwa sasa wako hoi kimaisha hivyo ushindi wa
CHADEMA katika nafasi mbalimbali za uongozi kutasaidia kuondoa kero
nyingi zilizopo.” Alisema

Alisema ana imani kubwa mwaka 2015 ambao ni mwaka wa uchaguzi mkuu
CHADEMA Sikonge itakuwa ni moto wa kuotea mbali na wananchi watakiunga
mkono.

No comments:

Post a Comment