Tuesday, December 4, 2012

TFDA yakutana na Wadau kujadili matokeo ya utafiti kuhusu sumu kuvu ( Aflatoxin)


Director General TFDA Mr. Hiiti Sillo akitoa maelezo mafupi juu ya warsha hiyo.
Sehemu ya washiriki katika warsha hiyo.
Mgeni rasmi, Kaimu Mganga Mkuu aw Serikali, Dr. Donan Mbando akifungua warsha hiyo jijini Dar Es Salaam.
Wadau wakifuatilia  jambo kwa makini
Wadau wa mkutano wakifuatilia utafiti juu ya simu kuvu (aflatoxin).

TFDA imekutana na wadau mbalimbali wanaohusika Moja kwa Moja katika masuala ya chakula nchini ili kujadili matokeo ya usafiri kuhusu sumu kuvu (aflatoxin) katika mahindi na karanga kwa Lengo la kupandwa mikakati ya kuitokomeza.

Akifungua warsha hiyo Mgeni rasmi ambaye ni Kaimu Mganga Mkuu wa Serikali, Dr. Donan Mmbando alisema kuwa anatambua mchango wa wadau mbalimbali na mikakati inayowekwa katika udhibiti wa tatizo hili la sumu kuvu ambalo lipo zaidi katika mahindi na karanga.

tatizo la Sumu kuvu bado halijaeleweka kwa kiasi kikubwa. Kwa mujibu wa wataalamu, Sumu kuvu katika nafaka  huweza kusababisha  matatizo ya Kansa ya ini, kushuka kwa kinga ya mwili na kuzaliwa na uzito mdogo.

Katika maelezo ya utangulizi Mkurugenzi Mkuu wa TFDA, Bw. Hiiti Sillo, aliwaeleza wajumbe kuwa, Warsha hii imekuja kufuatia utafiti uliofanyika nchi nzima na kupatikana kwa Hali halisi ya tatizo la sumu kuvu nchini na hivyo basi tukaona umuhimu wa kujadili matokeo ya hayo na wadau mbalimbali.  TFDA kwa kushirikiana na Taasisi ya kimarekani ijulikanayo Kama Abt Associates Pamoja na PACA wameandaa warsha hii ili kukubaliana na wadau mbalimbali katika Sekta ya chakula mikakati ya kutokomeza tatizo la sumu kuvu nchini.

Wadau walio shiriki ni Pamoja na wasindikaji vyakula, taasisi za Serikali, watafiti wa vyakula vya binadamu na mifugo na asasi za kimataifa.

No comments:

Post a Comment