Monday, December 3, 2012

UWANJA WA NDEGE TABORA WAWEKEWA LAMI KATIKA AWAMU YA KWANZA

Na Lucas Raphael,Tabora
 Baadhi ya mafundi wakiwa kazini katika kuhakikisha lami inawekwa uwanja huo wa ndege Tabora ili kuruhusu ndege kuruka na kutua masaa 24.
SERIKALI Mkoani TABORA imeridhishwa na maendeleo ya ujenzi wa Barabara ya kurukia Ndege kwa kiwango cha lami katika Uwanja wa Ndege wa TABORA ambao awamu ya kwanza itagharimu zaidi ya Shilingi Bilioni 11.6.

Mkuu wa Mkoa wa Tabora Fatma Mwassa ametembelea eneo la Mradi na kuelezea kuridhishwa kwake na kasi ya ujenzi wa Barabara ya uwanja huo yenye urefu wa mita 1900 ambayo kukamilika kwake itakuwa chachu ya kukua kwa uchumi wa Mkoa wa Tabora.

Mwassaa ameseama kwa muda mrefu wananchi wa Mkoa wa Tabora wamekosa usafiri wa anga kutokana na kufanyika kwa ujenzi wa uwanja huo ambao ulianza kufanyiwa matengenezo Desemba 15, mwaka jana na Kampuni ya ujenzi ya Sino hydro ya kutoka China.

Alisema ujenzi wa uwanja huo ukikamilika, ofisi yake itashiriki kuwahamasisha makampuni ya usafirishaji wa anga kupeleka ndege zao katika mkoa wa Tabora ambao una watu wengi wanaotumia usafiri huo wakiwemo Watalii wa uindaji wanatembelea mapori ya hifadhi ya wanyama pori mkoani humo.

Mhandisi Mshauri wa Mradi huu Isack Shayo alimweleza Mkuu wa mkoa kuwa mradi huo umegawanywa kwa awamu mbili, ambapo awamu ya kwanza ni ujenzi wa barabara ya lami yenye urefu wa Mita 1900.

Alisema awamu hii inatarajiwa kukamilika Mwezi Machi Mwaka 2013, lakini Ndege zinaweza kuanza kuutumia Uwanja huo Mwezi Januari mwakani.
Naye Meneja wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Mkoa wa Tabora Ezekia Mwalutende amesema ujenzi wa Uwanja unaonyesha matumaini makubwa, hivyo anatoa wito kwa Wasafirishaji wa Anga kuanza kufikiria kupeleka huduma hiyo Mkoani TABORA.

Baadhin ya Wananchi mbalimbali wa mkoa wa tabora waliozungunza na gazeti hili wamesema kukamilika kwa uwanja huo wa ndege kutasidia kukua kwa uchumu wa mkoa huu na hata kupata usafiri wa haraka hasa kwa wafanyabiashara wakubwa na wadogo.

Walisema kwamba usafiri huo utapunguza machungu ya ujenzi wa barabara unaondelea taratibu na sasa usafiri wa ndege kuwa jibu la matatizo ya usafiri katika mkoa huu ,ambapo kipindi cha masika tabbora inakuwa kisiwani.


Mwisho

No comments:

Post a Comment