Monday, December 3, 2012

WAIOMBA SERIKALI IWAJENGEE KITUO CHA POLISI


Na Lucas Raphael,Tabora
  

WANANCHI wa kata na kijiji cha Nsololo katika wilaya ya Uyui mkoani Tabora wameiomba Serikali kuwajengea kituo cha Polisi ili kukabiliana na matukio ya uhalifu katika kijiji chao

Mussa Malale na Juma Msoma ni wakazi wa kata hiyo , wamesema kwamba wameamua kutoa kilio hicho kqwa Serikali kutokana na kuongezeka kwa ,matukio ya uhalifu yakiwemo Ujambazi na pamoja na watu kuvuana mbao holela kutoka hifadhi ya msitu ya Nsololo.

Walisema kwamba kata hiyo yenye zaidi ya watu 18,248 Ambapo wanaume ni 8,215 na wanawake wanafikia 10,038 .

Wamesema kuwa kutokana na hali hiyo wakazi wa kijiji hicho wanaishi kwa hofu kubwa na kuongeza kwamba serikali ione umuhimu sasa wakuwajengea kituo hicho cha ili askari waeze kukabiliana kikamilifu na wahalifu hao.

Aidha wameeleza yakwamba kukosekana na kwa kituo hicho kimechangia kwa kiwango kikubwa kongezeka vitendo vua uhalifu ikiwemo wizi wa kutumia nguvu. 

Wananchi hao wamesema kuwa hivi karibuni watu wanaodhaniwa kuwa ni majambazi walivamia nyumbani wa mkazi mmoja waliyemtaja kwa jina moja la Mangi, alivamiwa na kuporwa pesa ya maozo ya dukani kwake.

Katika hatua nyingine wananchi hao wakiongozwa na Diwani wa kata hiyo Abas Kiberiti ameiomba Serikali ruhusu kutumia mbao zinazokamatwa na maafisa misitu zitumike kutengeneza madawati katika shule mbalimbali zenye upungufu wa vifaa hivyo.

Kiberiti amesema kuwa inashangaza kuona mbao zionazokamatwa na maafisa misitu kuwekwa stoo huku shule nyingi wanafunzi wake wanakosa madawati ya kukalia darasani.

Alisema kuwa iwapo mbao hizo zitatumika kutengeza madawati tatizo la upungufu wa madawati katika shule za msingi na kata huenda likamalizika kabisa.

Mwisho

No comments:

Post a Comment