Tuesday, December 4, 2012

WATAKIWA KUJISOMEA KWA BIDII




NA Lucas Raphael,Sikonge

MKUU wa Wilaya ya Sikonge mkoani Tabora ,Hanifa Selengu amewataka wanafunzi wa shule za sekondari wilayani humo,kusoma kwa bidii, ili waweze kujiongezea nafasi kufauru vizuri masomo yao.

Amesema kama wanafunzi hao watatumia muda wao mwingi kujisomea watajiongezea nafasi kubwa ya ufauru katika masomo yao na hivyo kuhimili vilivyo maisha ya dunia ya sasa ya Sayansi na teknolojia.

Mkuu huyo wa wilaya ya sikonge amewaeleza wanafunzi hao kwamba, siri kubwa ya mafanikio katika masomo ni kusoma kwa bidii na kutoa mfano kuwa mtu akijisomea muda mwingi anajihakikishia kuandaa maisha ya baadaye. 

Silengu ameyasema wakati akiweka jiwe la msingi la ujenzi wa shule ya Sekondari Ugunda iliyopo nje kidogo na mji wa sikonge. 

Awali mkuu wa shule ya ugunda ,Merwa Mbiha amesema kuwa mradi huo ukikamilika ujenzi wake utagharimu kiasi cha shilingi milioni 23,854,000.

Amesema katika ujenzi huo Serikali kuu imechangia kiasi cha shilingi milioni 13,900,000, wakati Halmashauri imetoa shilingi milioni 7,900,000 huku wananchi nao wakichangia nguvu kazi ya shilingi milioni 2.4.

Hata hivyo mkuu huyo wa shule ugunda amemweleza mkuu wa wilaya kuwa, shule yake inakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo uhaba wa maji, ukosefu wa mabweni ya kulala wananfunzi na ukosefu wa nishati ya umeme kwa ajili ya matumizi shuleni hapo.

Kwa upande wake mkuu wa wilaya hiyo ,Hanifa Silengu amesema kuwa Serikali ya chama cha mapinduzi CCM inatambua changamoto zinazozikabili shule mbalimbali hapa nchini na kuhahidi kuzishughulikia haraka iwezekanavyo.

Amemwagiza mkurugenzi wa Halmashauri hiyo ,Paul Nkulila kuhakikisha wanatatua haraka matatizo katika shule hiyo ili wanafunzi waeze kusoma katika mazingira mazuri.

Mwisho



No comments:

Post a Comment