Tuesday, December 4, 2012

ZIARA YA WAZIRI WA KILIMO, USHIRIKA NA CHAKULA MH.CHRISTOPHA CHIZA, KWA KNCU (1984) LTD MKOANI KILIMANJARO



 Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Mh. Christopha  Chiza(katikati), akisisitiza jambo katika kikao hicho  cha uongozi wa KNCU.  Pia waziri aliomba KNCU ikubali kuendelea kupokea wanaushirika toka maeneo mengine nchini,na nje ya nchi, wanaopenda kujifunza zaidi kuhusu mbinu KNCU inazotumia, inachokifanya kuwa chama kikuu kikongwe Afrika, chenye takribani miaka 80 tangu kuuanzishwa kwake.   Kulia ni Mwenyekiti wa Bodi Bw.Maynard Swai, na kushoto ni mkuu wa wilaya ya Moshi, Dkt.Ibrahim Msengi.

 Bw.Maynard Swai (kulia)akimkabidhi zawadi, kwa niaba ya KNCU moja ya wasaidizi wa Mh.Waziri.
Bw.Maynard Swai, akiwasilisha hotuba kwa Mh.Waziri, juu ya shuhuli za KNCU ikiwamo mradi wa Afya unaoendeshwa na chama hiki, ambao ni mahususi kwa wakulima ambao ni wanachama wa KNCU.
 Wafanyakazi wa KNCU (1984)Ltd, pamoja na wajumbe wa bodi ya KNCU Bw.Martin Malya (mwenyemiwani) na Bw.Silayo(wa pili kulia),wakifuatilia jambo katika mkutano huo.
 Wafanyakazi wa KNCU (1984) Ltd, wakila chakula cha pamoja na Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Coffee Tree Hotel. 

Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Mh. Christopha  Chiza(kulia) akikaribishwa na Mwkt wa KNCU Maynard Swai (kushoto), pamoja na mkuu wa Wilaya ya Moshi(katikati) Dkt.Ibrahim Msengi, katika hoteli ya KNCU ya Coffee Tree Hotel, mjini Moshi, tarehe 30 Nov. 2012

No comments:

Post a Comment