Sunday, December 2, 2012

MAHAKAMA HAZIWATENDEI HAKI WATUHUMIWA



Na Lucas Raphael,Tabora

Wananchi mkoani Tabora wamezilalamikia mahakama mkoani hapa kwa kuchelewesha kutoa hukumu katika mashauri mbalimbali yanayo wakabili watuhumiwa walijazana katika mahabusu mkoani Tabora.

Hayo yalisemwa na wajumbe wa kamati ya maadili na nidhamu ya mahakama  ngazi ya mkoa katika kikao cha maadili kilichoketi mwishoni mwa wiki kilichoketi katika ukumbi wa mikutano wa mtemi Isike 

Kamanda wa Takukuru mkoa wa Tabora,Leonard Mtalai ambaye ni  
mjumbe wa kamati hiyo alisema kuwa baadhi ya mahakama zimekuwa zikichelewesha kesi za watuhumiwa na kusababisha msongamano mkubwa wa mahabusu katika magereza.

Alisema kuwa muda muafaka umefika kwa vyombo hivyo kutoa haki za wananchi mapema ikiwa na upelelezi kwa jeshi la polisi kufanyika mapema ili hukumu  kwa haraka zifanyike tofauti na sasa.

Kikao hicho kikihudhuriwa na wadau mbalimbali mwenyekiti wa kikao hicho alikuwa ni mkuu wa mkoa wa Tabora Fatuma Mwassa alisema kuwa vyombo hivyo vya mahakama vitoe hukumu mapema kwa kuzingatia utendaji haki kwa kila mtuhumiwa.

Alisema mahakama hizo zinasheria zake ambazo zinafuatwa na kuheshimika hivyo kanuni hizo na sheria zifuatwe ili wananchi wapate haki zao kwa muda muafaka.

Mwenyekiti huyo aliongeza kuwa mpango maalumu wakuzungumza na Halmashauri za wilaya zichangie katika kukarabati majengo ya mahakama ikiwa na makazi ya watumishi wa mahakama hizo unatarajiwa kuanza.

Hata hivyo katika kikao hicho hakimu mkazi hakuweza kupatikana ili kutoa ufafanuzi zaidi wa kuchelewesha mashauri ya watuhumiwa yanayosababisha msongamano wa watuhumiwa magerezani ambao wapo mahabusu. 

Hata hivyo Ofisa magereza wa mkoa hakuweza kufika katika kikao hicho ilikutoa ufafanuzi zaidi juu ya msongamano wa magereza mkoani hapa ambapo gereza la nzega linadaiwa kuwa na msongamano mkubwa wa watuhumiwa kuliko uwezo wake.

Mwisho.

No comments:

Post a Comment