NHIF YASHIRIKI VYEMA MAADHIMISHO YA SIKU YA UKIMWI DUNIANI MKOANI LINDI
Mwakilishi
wa Mfuko wa bima ya Afya (NHIF) mkoani Lindi Bi, Fortunata Raymond wa
tatu kutoka kulia pamoja na wafanyakazi wenzake, wakionyesha cheti
walichokabidhiwa na kamati ya maandalizi ya maadhimisho ya siku ya
ukimwi Duniani yaliyofanyika kwenye uwanja wa Ilulu Mjini Lindi jana,
kutokana na ushiriki wao kwenye maadhimisho hayo.
Kazi kubwa iliyofanywa na maafisa
wa (NHIF) ilikuwa kuelimisha wananchi na kuwapa maelezo wananchi juu ya
umuhimu wa kujiunga na mifuko ya afya ya jamii ili kuboresha afya zao
pamoja na familia zao.
Mwakilishi
wa NHIF mkoani Lindi Bi. Fortunata Raymond wa tatu kutoka kulia
akiongoza wafanyakazi wa mfuko huo kupita mbele ya Rais Jakaya Kikwete
kwa maandamano wakiingia kwenye uwanja wa Ilulu kwa maadhimisho ya siku
ya ukimwi duniani yaliyofanyika jana mjini Lindi
Wasanii
wa vichekesho wanaojulukana kama Shoti na Hasara wakiaga mashabiki wao
mara baada ya kuwavunja mbavu wananchi waliohudhuria katika maadhimisho
hayo kwenye uwanja wa Ilulu mjini Lindi jana.
No comments:
Post a Comment